Ufini
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: none | |||||
Wimbo wa taifa: Maamme (Kifini) Vårt land (Kiswidi) ("Nchi yetu" Kiswahili) |
|||||
Mji mkuu | Helsinki |
||||
Mji mkubwa nchini | Helsinki | ||||
Lugha rasmi | Kifini, Kiswidi | ||||
Serikali
Rais
Prime Minister |
Jamhuri2 Tarja Halonen Matti Vanhanen |
||||
Uhuru imetangazwa |
December 6, 1917 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
338,145 km² (ya 64) 9.4 |
||||
Idadi ya watu - 2006 kadirio - 2000 sensa - Msongamano wa watu |
5,265,926 (ya 112) 5,181,115 15/km² (ya 190) |
||||
Fedha | Euro (€)1 (EUR ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
EET (UTC+2) EEST (UTC+3) |
||||
Intaneti TLD | .fi | ||||
Kodi ya simu | +358 |
||||
1Prior to 1999: Finnish markka 2Semi-presidential system |
Ufini (Kifini: Suomi) ni nchi ya Skandinavia au Ulaya ya Kaskazini. Pia ni nchi mwanachama wa Umoja ya Ulaya. Imepakana na Norway upande wa Kaskazini, Urusi upande wa mashariki na Uswidi upande wa magharibi. Ng'ambo ya Baltiki iko Estonia na watu wake hutumia lugha iliyo karibu sana na Kifini.
Mji Mkuu iko Helsinki. Nchi ina wakazi milioni tano tu katika eneo la 338,000 km² hivyo ni kati ya nchi za Ulaya zenye msongamano wa watu mdogo. Sehemu kubwa ya eneo lake ni misitu tu.
[edit] Watu
Kuna jumuiya tatu katika Ufini: Wafini wenyewe ambao ni 92% ya wakazi wote. Waswidi wako katika kusini ya nchi kwa jumla takriban 5.5% ya wakazi. Hasa visiwa vya Aland kuna Waswidi watupu walio na hali ya kujitawala ndani ya Ufini. Wakazi asilia ni Wasami wako kaskazini tu. Maisha yao ni wavindaji na wafugaji. Wako wachache, jumla yao haifiki 1% ya wakazi wote.
Lugha rasmi ni Kifini na Kiswidi. Lugha ya Kifini ina asili ya Asia ya kati haina uhusiano na lugha nyingine ya Kiulaya isipokuwa lugha ya Waestonia inafanana. Inaonekana ya kwamba mababu wa Wafini na Waestonia walihama pamoja wakiwa na lugha ileile zamani lakini sasa ni lugha mbili kwa sababu hawakuwa na mawasiliano kati yao kwa muda mrefu.
Wakazi wenye lugha ya Kiswidi wako kusini ya nchi kwa sababu Ufini ilitawaliwa na Uswidi kwa karne nyingi. Katika karne hizi walikuwepo Waswidi waliohamia Ufini lakini kuna pia Wafini walioanza kutumia Kiswidi pekee. Hasa kwenye visiwa vya Aland Kiswidi ni lugha ya pekee. Lakini Waswidi wa Ufini wanajisikia wako Wafini kisiasa. Viongozi wa kwanza baada ya uhuru wa Ufini mwaka 1917 walikuwa Waswidi Wafini.
[edit] Waja
Nchi na maeneo ya Ulaya | |
---|---|
Albania | Andorra | Austria | Belarus | Bosnia na Herzegovina | Bulgaria | Kroatia | Denmark | Estonia | Ufaransa | Hungaria | Iceland | Ireland | Italia | Latvia | Liechtenstein | Lithuania | Luxemburg | Masedonia | Malta | Moldova | Monako | Norway | Poland | Romania | San Marino | Serbia na Montenegro3 | Slovakia | Slovenia | Hispania | Ubelgiji | Uceki | Ufini | Ugiriki | Ujerumani | Uholanzi | Ureno | Urusi1 | Uswidi | Uswisi | Ukraine | Uingereza | Vatikan
Maeneo ya Ulaya ya kujitawala chini ya nchi nyingine: Visiwa vya Faroe | Gibraltar | Guernsey | Jan Mayen | Jersey | Isle of Man | Svalbard Nchi za Asia ambazo ni mwanachama wa baraza la Ulaya au vyombo vingine vya Ulaya: Armenia2 | Azerbaijan1 || Cyprus2 | Georgia1 | Kazakhstan1 | Uturuki1 Nchi zisizokubaliwa na umma wa kimataifa: Abkhazia | Nagorno-Karabakh2 | Ossetia ya Kusini | Transnistria | Jamhuri ya Kituruki ya Cyprus ya Kaskazini2 Maelezo: (1) nchi ya kimabara katika Asia na Ulaya; (2) nchi katika eneo la Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) lakini kiutamaduni huhesabiwa kuwa sehemu ya Ulaya; (3) Inaelekea kugawiwa kuwa nchi mbili za Serbia na Montenegro |