Bosnia na Herzegovina
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: -- | |||||
Wimbo wa taifa: "Intermeco" | |||||
Mji mkuu | Sarajevo |
||||
Mji mkubwa nchini | Sarajevo | ||||
Lugha rasmi | Kibosnia, Kikroatia, Kiserbia | ||||
Serikali
Maraisi wa Bosnis na Herzegovina
Mwenyekiti wa halmashauri ya mawaziri |
Jamhuri Haris Silajdžić1 (Mbosnia) Nebojša Radmanović (Mserbia) Željko Komšić (Mkroatia) Adnan Terzić |
||||
Uhuru Ilitambuliwa |
6 Aprili 1992 |
||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
51,197 km² (128) -- |
||||
Idadi ya watu - Julai 2006 kadirio - 1991 sensa - Msongamano wa watu |
4,498,9762 (ya 1273) 4,377,033[1] 76/km² (ya 1163) |
||||
Fedha | Convertible mark pamoja na Euro ( BAM4 ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) |
||||
Intaneti TLD | .ba | ||||
Kodi ya simu | +387 |
||||
1 Maraisi watatu wanaobadilishanan 2 Kadirio ya CIA World Factbook [2]. |
Bosnia na Herzegovina (Bosna i Hercegovina au Босна и Херцеговина ) ni nchi ya Ulaya kusini mashariki kwenye rasi ya Balkani. Ilikuwa sehemu ya Yugoslavia hadi 1992. Eneo lake ni 51,129 km² linalokaliwa na wakazi milioni nne. Mara nyingi huitwa kwa kifupi "Bosnia" tu na watu wake "Wabosnia". Mji mkuu ni Sarayevo.
Kati ya wakazi kuna vikundi vitatu vinavyotofautiana kiutamaduni na kidini: Wabosnia (48%), Waserbia (37%) na Wakroatia (13%). Wanadai ya kwamba lugha zao ni tofauti lakini hali halisi ni lugha ileile ya Kislavoni. Wakati wa Yugoslavia iliitwa "Kiserbokroatia". Tofauti ziko kwa sababu Wabosnia hutazamiwa kuwa Waislamu, Waserbia kuwa Wakristo Waothodoksi na Wakroatia kuwa Wakristo Wakatoliki.
Nchi ina vitengo viwili: Shirikisho la Bosnia na Herzegovina linalounganisha maeneo ya Waislamu na Wakatiliki na Republika Srpska au eneo la Waserbia Waorthodoksi.
[edit] Historia
Bosnia ilitokea kama eneo la pekee wakati za enzi za kati chini ya utawala wa Dola la Uturuki. Jina la Bosnia limetokana na mto Bosna. Jina la Herzegovina lilitokana na watemi wa kusini katika eneo la mji wa Mostar waliotumia cheo cha Kijerumani cha "Herzog" na eneo la lilitwa "nchi ya Herzog" au "Herzegovina".
Utawala wa Kiislamu ulisababisha kugeuka kwa sehemu kubwa ya wakazi kuwa Waislamu walioendlea kutumia lugha yao ya Kislavoni. Wakati wa kudhoofika kwa Dola la Uturuki katika karne ya 19 utawala wa nchi ulifika mkonono wa Austria-Hungaria. Vita kuu ya kwanza ya dunia ilisababishwa mjini Sarayevo kutokana na mauaji ya mfalme mteule wa Austria na mke wake.
Kati ya 1918 na 1992 Bosnia na Herzegovina ilikuwa jimbo la Yugoslavia. Baada ya uhuru ilitokea vita kali kwa sababu sehemu ya Waserbia na wa Wakroatia walitaka kuunganisha nchi au sehemu zake na Serbia au Kroatia. Wakazi wengi walifukuzwa nyumbani kwao kufuatana na maeneo ambako wanamigambo wa Waserbia au Wakroatia walitawala kufukuzo waote wengine.
Jumuiya ya kimataifa iliingilia kati na kuwalazimisha washiriki kukubali amani katika mkataba wa Dayton wa 1995. Mamlaka kuu haiko mkonono wa serikali ya wenyeji lakini mkononi mwa Kamishna Mkuu kwa Bosnia na Hercegovina anayeteuliwa na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya. Ana mamlaka ya kubatilisha sheria zilizoamuliwa na bunge pia kuachisha mawaziri kazi.
[edit] Viungo vya Nje
Nchi na maeneo ya Ulaya | |
---|---|
Albania | Andorra | Austria | Belarus | Bosnia na Herzegovina | Bulgaria | Kroatia | Denmark | Estonia | Ufaransa | Hungaria | Iceland | Ireland | Italia | Latvia | Liechtenstein | Lithuania | Luxemburg | Masedonia | Malta | Moldova | Monako | Norway | Poland | Romania | San Marino | Serbia na Montenegro3 | Slovakia | Slovenia | Hispania | Ubelgiji | Uceki | Ufini | Ugiriki | Ujerumani | Uholanzi | Ureno | Urusi1 | Uswidi | Uswisi | Ukraine | Uingereza | Vatikan
Maeneo ya Ulaya ya kujitawala chini ya nchi nyingine: Visiwa vya Faroe | Gibraltar | Guernsey | Jan Mayen | Jersey | Isle of Man | Svalbard Nchi za Asia ambazo ni mwanachama wa baraza la Ulaya au vyombo vingine vya Ulaya: Armenia2 | Azerbaijan1 || Cyprus2 | Georgia1 | Kazakhstan1 | Uturuki1 Nchi zisizokubaliwa na umma wa kimataifa: Abkhazia | Nagorno-Karabakh2 | Ossetia ya Kusini | Transnistria | Jamhuri ya Kituruki ya Cyprus ya Kaskazini2 Maelezo: (1) nchi ya kimabara katika Asia na Ulaya; (2) nchi katika eneo la Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) lakini kiutamaduni huhesabiwa kuwa sehemu ya Ulaya; (3) Inaelekea kugawiwa kuwa nchi mbili za Serbia na Montenegro |