Monako
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: Deo Juvante (Kilatini: Kwa msaada wa Mungu) |
|||||
Wimbo wa taifa: Hymne Monégasque | |||||
Mji mkuu | Monaco1 |
||||
Eneo lenye watu wengi | Monte Carlo | ||||
Lugha rasmi | Kifaransa na Kimonako2 | ||||
Serikali
Mtemi
|
Ufalme mwenye katiba (Utemi) Albert II |
||||
Uhuru Watemi wa Grimaldi kukubaliwa na mfalme wa Ufaransa kuwa wanajitegemea |
1489 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
1.95 km² (193rd) 0.0% |
||||
Idadi ya watu - 2006 kadirio - 2000 sensa - Msongamano wa watu |
35,656 (ya 210) 32,020 18,285/km² (ya 1) |
||||
Fedha | Euro (EUR ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) |
||||
Intaneti TLD | .mc | ||||
Kodi ya simu | +377 |
||||
1Monako ni dola-mji. 2Kiitalia hutumiwa pia na wengi |
Utemi wa Monako (Kifaransa: Principauté de Monaco; Kimonako: Principatu de Munegu) au "Monako" kwa kifupi ni kati ya nchi ndogo kabisa duniani. Hali halisi ni dola-mji ambako mji ni sawa na nchi na dola lote.
Contents |
[edit] Eneo
Eneo lake ni kanda nyembamba ufukoni wa bahari ya Mediteranea tu lenye urefu wa 4km pekee karibu na mpaka wa Ufaransa na Italia lakini ndani ya Ufaransa. Baada ya kupata nchi kavu mpya kwa kujenga baharini eneo limeongezeka 40 ha kuwa 195 ha au 1.95 km². Kuna mitaa sita mjini au nchini ndiyo Monte Carlo, La Condamine, Fontvieille, Le Larvotto, Les Moneghetti na Monaco-Ville.
Kuna nchi moja ndogo duniani kushinda Monako ambayo ni mji wa Vatikano. Hakuna nchi yenye msongamano mkubwa duniani kuliko Monako ikiwa na wakazi zaidi ya 18,000 kwa kilomita ya mraba.
[edit] Wakazi
Lugha inayotumika hasa ni Kifaransa ambayo ni lugha rasmi. Sehemu ya wananchi bado hutumia Kimonako ambayo ni lugha kati ya Kifaranya ya Kusini na Kiitalia ya Kaskazini. Monako ina dini rasmi ambayo ni Ukristo wa Kikatoliki.
[edit] Wananchi wachache, wageni wengi
Idadi ya wakazi ni takriban 35,000 ambao 5,070 au 16% ya wakazi wote ni wananchi na wengine wageni wanaoishi mjini. 47% ya wakazi ni Wafaransa, 16% Waitalia na wengine 21% ni raia ya mataifa 125 mbalimbali.
[edit] Nchi ya matajiri wengi
Monako haina kodi ya mapato. Hali hii imesababisha matajiri wengi kutoka nchi mbalimbali kuhamia nchini. Hivyo Monako ni nchi yenye asilimia kubwa ya mamilionea kulingana na idadi ya wakazi wote kuliko nchi yoyote duniani.
[edit] Historia
Historia ya Monako imekuwa sawa na historia ya familia ya Grimaldi tangu mwanzo wake. Akina Grimaldi walikuwa matajiri katika mji wa Genova (Italia) waliopaswa kukimbia nchi wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1296 BK. Walinunua cheo cha kitemi pamoja na maeneo madogomadogo ya utawala katika Italia ya Kaskazini hadi Ufaransa Kusini. Kati ya maeneo haya yote ni Monako pekee iliyobaki mkononi mwao tangu kuondoa mji mkononi wa Genova mwaka 1419. Watemi wa Grimaldi walifaulu kwa siasa yenye busara kupata kibali cha Wafalme wa Ufaransa kuwa eneo la kujitegemea bila mamlaka ya kifalme juu yao. Wakati ule palikuwapo na nchi nyingi ndogo sana za aina hii katika Ulaya hasa Italia na Ujerumani.
Busara ya Wagrimaldi iliwawezesha kutunza uhuru wao katika karne zilizofuata hasa wakijenga uhusiano mzuri mara na huyu mara na mwingine kati ya majirani wakubwa. Kati ya 1425 hadi 1641 Wagrimaldi waliweka nchi yao chini ya ulinzi wa Hispania wakiwalipia Wahispania pesa kwa kuweka kikosi cha wanajeshi katika boma la Monako. Tendo hili lilikuwa utetezi dhidi ya wafalme wa Ufaransa ambao wakati mwingine walielekea kumeza nchi ndogo. Baada ya kuchoka na Wahispania walifanya mapatano na Wafaransa waliowalazimisha Hispania ya kuondoka.
Wakati wa mapinduzi ya Ufaransa mwaka 1789 utawala wa kifalme na kitemi ulifutwa kabisa Ufaransa na serikali ya mapinduzi hayakuheshimu tena mapatano ya kukubali uhuru wa eneo la akina Grimaldi. Lakini baada ya kipindi cha Napoleon aliyerithi matunda ya mapinduzi mataifa ya Ulaya kwenye mkutano wa Vienna mwaka 1815 yalipatana kurudisha hali jinsi ilivyowahi kuwa awali. Wagrimaldi walirudi Monako wakiendelea kutawala hadi leo.
[edit] Nchi lindwa ya Ufaransa
Tangu 1918 Monako ni nchi lindwa ya Ufaransa yenye uhuru katika mambo ya ndani lakini kwa masharti kuhusu mambo ya nje. Ufaransa ina haki ya kutaja majina kwa ajili ya nafasi za Mkuu wa Polisi na Mwanasheria Mkuu. Kiuchumi ni sehemu ya Ufaransa isipokuwa ina sheria zake juu ya kodi. Hivyo ni pia sehemu ya eneo la forodha la EU bila kuwa mwanachama wa EU. Lakini Monako ni mwanachama wa UM pia wa Halmashauri ya Ulaya.
Mkataba wa 1918 una kipengelea ya kwamba uhuru wa nchi utakwisha kama hakuna mrithi tena wa familia ya Grimaldi atakayechukua cheo cha mtemi. Mtoto wa kupanga atakubaliwa kama mrithi.
[edit] Viungo vya Nje
- Monaco Guide for Monaco
- Template:Wikitravel
- Official website
- http://eudocs.lib.byu.edu/index.php/History_of_Monaco:_Primary_Documents History of Monaco: Primary documents]
- Official website of the Prince's Palace of Monaco
- Official website for Tourism
- Monaco Guide for Monaco
- In the House of Grimaldi, a reprint of a 1993 article from the author's personal website
- Monaco Eye: Unofficial Guide for Visitors to Monaco
- Satellite Map of Monaco with Grand Prix track
- Order of the doctors of Monaco
- European Business article
- Monaco photo gallery
- Street map of Monaco
Nchi na maeneo ya Ulaya | |
---|---|
Albania | Andorra | Austria | Belarus | Bosnia na Herzegovina | Bulgaria | Kroatia | Denmark | Estonia | Ufaransa | Hungaria | Iceland | Ireland | Italia | Latvia | Liechtenstein | Lithuania | Luxemburg | Masedonia | Malta | Moldova | Monako | Norway | Poland | Romania | San Marino | Serbia na Montenegro3 | Slovakia | Slovenia | Hispania | Ubelgiji | Uceki | Ufini | Ugiriki | Ujerumani | Uholanzi | Ureno | Urusi1 | Uswidi | Uswisi | Ukraine | Uingereza | Vatikan
Maeneo ya Ulaya ya kujitawala chini ya nchi nyingine: Visiwa vya Faroe | Gibraltar | Guernsey | Jan Mayen | Jersey | Isle of Man | Svalbard Nchi za Asia ambazo ni mwanachama wa baraza la Ulaya au vyombo vingine vya Ulaya: Armenia2 | Azerbaijan1 || Cyprus2 | Georgia1 | Kazakhstan1 | Uturuki1 Nchi zisizokubaliwa na umma wa kimataifa: Abkhazia | Nagorno-Karabakh2 | Ossetia ya Kusini | Transnistria | Jamhuri ya Kituruki ya Cyprus ya Kaskazini2 Maelezo: (1) nchi ya kimabara katika Asia na Ulaya; (2) nchi katika eneo la Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) lakini kiutamaduni huhesabiwa kuwa sehemu ya Ulaya; (3) Inaelekea kugawiwa kuwa nchi mbili za Serbia na Montenegro |