Denmark
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: hakuna | |||||
Wimbo wa taifa: Der er et yndigt land (kitaifa); Kong Christian (kifalme) |
|||||
Mji mkuu | Kopenhagen |
||||
Mji mkubwa nchini | Kopenhagen | ||||
Lugha rasmi | Kidenmark1 | ||||
Serikali
Malkia
Waziri Mkuu |
Ufalme wa kikatiba Margrethe II Anders Fogh Rasmussen |
||||
Kuungana kwa nchi {{{established_events}}} |
mnamo 980 BK | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
43,094 km² (ya 1341) 1.6%1 |
||||
Idadi ya watu - 2005 kadirio - 2006 sensa - Msongamano wa watu |
5,431,000 (ya 109) 5,450,661 126/km² (ya 783) |
||||
Fedha | Kroner (DKK ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET3 (UTC+1) CEST3 (UTC+2) |
||||
Intaneti TLD | .dk1 | ||||
Kodi ya simu | +453 |
||||
1 Habari zote za Denmark bila Faroe na Greenland. |
Denmark (pia Denmaki (au Denimaki au Denmak) - Kidenmark: Kongeriget Danmark) ni ufalme ya Ulaya ya Kaskazini. Ni nchi ndogo kati ya nchi za Skandinavia. Imepakana na Ujerumani kwa kusini na kuzungukwa na maji pande tatu. Kaskazini yake iko Norway ng'ambo ya mlango wa bahari ya Skagerak, mashariki iko Uswidi ng'ambo ya Kattegat na Oresund. Bahari ya Kaskazini iko upande wa magharibi, Baltiki inaanza kwenye visiwa vikuu vya Denmark.
[edit] Eneo
Denmark ina eneo la 43.000 km². Theluthi ya eneo hili ni kwenye visiwa 443 vya Denmark ambavyo 76 kati vyao vinakaliwa na watu.
Rasi ya Jutland ni sehemu kubwa ya eneo. Jutland ni Denmark bara. Ina urefu wa 300 km kuelekea kaskazini kutoka mpaka wa Ujerumani hadi ncha yake kwa Skagen.
Kwa jumla Denmark iko tambarare. Mlima wa juu ina kimo wa 170 m juu ya UB pekee.
Visiwa vikubwa ni Funen (Fyn), Zealand (Sjælland) na Bornholm (Bornholm).
Greenland na visiwa vya Faroe ni sehemu ya ufalme wa Denmark lakini zinajitawala.
[edit] Historia
(angalia makala "Historia ya Denmark")
Wadenmark wa kwanza waliojulikana katika historia kwa jina ni makabila ya Wakimbri na Wateutonia waliohamia hadi Ulaya ya kusini wakati wa njaa mnamo mwaka 113 KK.
Katika karne za 8 hadi ya 11 BK majambazi wa baharini kutoka Denmark na Norway waliogopwa kote Ulaya kwa jina la "Waviking". Walivamia pia Uingereza mara kwa mara na kujenga makao huko. Tangu mwaka 793 walitawala eneo la Danelag (au: Danelaw) iliyoenea katika kaskazini na kaskazini-mashariki ya Uingereza wa leo.
Katika karne ya tisa na karne ya kumi maeneo madogo yaliunganishwa. Wafalme wa kwanza wanaojulikana kutawala Denmark yote walikuwa Garm Mzee na Harald Jino Buluu (mnamo mwaka 980 BK). Harald alikuwa mfalme wa kwanza wa kupokea Ukristo wa kikatoliki. Denmark ikawa nchi yenye nguvu katika Skandinavia na kwenye pwani za Baltiki.
Kati ya 1397 hadi 1521 nchi zote za Skandinavia ziliunganishwa katika maungano ya kifalme chini ya wafalme wa Denmark ilhali kila nchi ilijitawala katika mambo ya ndani. Baada ya Uswidi kujitenga na umoja huu Norway iliendela kuwa chini ya Denmark hadi mwaka 1814.
Mwaka 1537 Denmark ilijiunga na mwendo wa Matengenezo ya Kanisa na kanisa la Kiluteri likawa dini rasmi nchini. Denmark ilikuwa kati ya nchi muhimu sana ya Uluteri.
Baada ya vita za Napoleoni Denmark iliondolewa utawala wa Norway iliyounganishwa na Uswidi mwaka 1814. Lakini koloni za Greenland, Iceland, Faroe na visiwa vya Karibi zilibaki kwa nchi.
Karne ya 19 ilileta fitina na Ujerumani juu ya utawala wa Schleswig na Holstein. Baada ya vita ya 1864 Denmark ilipaswa kuacha majimbo haya mawili kwa Ujerumani.
Denmark haikushiriki katika Vita Kuu ya Dunia ya Kwanza lakini ilirudishwa sehemu ya kaskazini ya jimbo la Schleswig.
Wakati wa Vita Kuu ya Dunia ya Pili Denmark ilivamiwa na Ujerumani mwaka 1940 hadi 1945. Wakati wa vita Iceland iliamua kutangaza uhuru wake. 1948 mara baada ya vita visiwa vya Faroe vilipewa madaraka ya kujitawala lakini vilibaki ndani ya umoja na Denmark. Koloni ya Greenland ilipewa madaraka haya mwaka 1979.
Denmark ikawa kati ya nchi zilizounda UM na pia NATO. Mwaka 1973 ikajiunga na Jumuiya ya Ulaya (sasa: Umoja wa Ulaya).
[edit] Waja
Makala hiyo kuhusu "Denmark" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Denmark kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |
Nchi na maeneo ya Ulaya | |
---|---|
Albania | Andorra | Austria | Belarus | Bosnia na Herzegovina | Bulgaria | Kroatia | Denmark | Estonia | Ufaransa | Hungaria | Iceland | Ireland | Italia | Latvia | Liechtenstein | Lithuania | Luxemburg | Masedonia | Malta | Moldova | Monako | Norway | Poland | Romania | San Marino | Serbia na Montenegro3 | Slovakia | Slovenia | Hispania | Ubelgiji | Uceki | Ufini | Ugiriki | Ujerumani | Uholanzi | Ureno | Urusi1 | Uswidi | Uswisi | Ukraine | Uingereza | Vatikan
Maeneo ya Ulaya ya kujitawala chini ya nchi nyingine: Visiwa vya Faroe | Gibraltar | Guernsey | Jan Mayen | Jersey | Isle of Man | Svalbard Nchi za Asia ambazo ni mwanachama wa baraza la Ulaya au vyombo vingine vya Ulaya: Armenia2 | Azerbaijan1 || Cyprus2 | Georgia1 | Kazakhstan1 | Uturuki1 Nchi zisizokubaliwa na umma wa kimataifa: Abkhazia | Nagorno-Karabakh2 | Ossetia ya Kusini | Transnistria | Jamhuri ya Kituruki ya Cyprus ya Kaskazini2 Maelezo: (1) nchi ya kimabara katika Asia na Ulaya; (2) nchi katika eneo la Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) lakini kiutamaduni huhesabiwa kuwa sehemu ya Ulaya; (3) Inaelekea kugawiwa kuwa nchi mbili za Serbia na Montenegro |