Asia
From Wikipedia
Asia ni bara kubwa kabisa kuliko mabara yote mengine ya dunia. Bara hili lina eneo la kilomita 44,579,000 muraba (maili 17,212,000 muraba), yaani inakalia asilimia 30% ya ardhi yote. Wakaazi wa bara la Asia ni 3,701,000,000 kwa mujibu wa makisio 2003.
Bara la Asia lina nchi 44 na visiwa mbali mbali vya madola tofauti tofauti. Mlima mrefu kabisa ulimwenguni ambao ni mlima wa Everesti wenye urefu wa mita 8,850 (futi 29,035) ulioko Nepal pia uko kwenye bara hili. Kadhalika, nchi zenye wakaazi wengi zaidi ulimwenguni China na India pia ziko kwenye bara hili.
Ziwa kubwa kabisa ulimwenguni, bahari ya Kazwini (Caspian Sea) lenye eneo la kilomita 394,299 muraba (maili 152,239 muraba) vile vile liko baina ya nchi hizi: Azerbaijan, Urusi, Kazakhstan, Turkmenistan, Uajemi kwenye bara hili.
Inawezekana kuganwanya bara la Asia katika sehemu zifuatazo:
Contents |
[edit] Asia ya Kati
Sehemu hiyo ya Asia ina nchi saba:
- Afghanistan
- Kazakhstan
- Kirgizistan
- Mongolia
- Tajikistan
- Turkmenistan
- Usbekistan
[edit] Asia ya Kaskazini
Sehemu hiyo ya Asia ina sehemu ya nchi moja tu:
[edit] Asia ya Mashariki
Sehemu hiyo ya Asia ina nchi nne:
- Uchina (pamoja na Taiwan)
- Japani
- Korea Kaskazini
- Korea Kusini
[edit] Asia ya Kusini-Mashariki
Sehemu hiyo ya Asia ina nchi kuminamoja
- Brunei
- Indonesia
- Kamboja
- Laos
- Malaysia
- Myanmar (zamani iliitwa Burma)
- Philippines
- Singapur
- Thailand (zamani iliitwa Siam)
- Timor Mashariki
- Vietnam
[edit] Asia ya Kusini
Sehemu hiyo ya Asia ina nchi saba:
[edit] Asia ya Magharibi
- Armenia
- Azerbaijan
- Bahrain
- Georgia
- Irak
- Israel
- Yemeni
- Yordan
- Qatar
- Kuwait
- Libanon
- Omani
- Palestina
- Shamu (au: Syria)
- Ufalme wa Arabia
- Uajemi (au Iran au Persia)
- Uturuki
Categories: Bara | Asia