Iceland
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: (hakuna) | |||||
Wimbo wa taifa: Lofsöngur | |||||
Mji mkuu | Reykjavík |
||||
Mji mkubwa nchini | Reykjavík | ||||
Lugha rasmi | Kiiceland | ||||
Serikali
Rais
Waziri Mkuu |
Jamhuri Ólafur Ragnar Grímsson Geir Hilmar Haarde |
||||
Uhuru kujitawala Jamhuri |
1. 12. 1918 17. 06. 1944 |
||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
103,000 km² (ya 107) 2.7 |
||||
Idadi ya watu - Julai 2006 kadirio - Disemba 1970 sensa - Msongamano wa watu |
297,139 (ya 178) 204,930 2.89/km² (ya 222) |
||||
Fedha | Króna ya Iceland (ISK ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
GMT (UTC+0) None (UTC) |
||||
Intaneti TLD | .is | ||||
Kodi ya simu | +354 |
Iceland (pia: Aisilandi, Isilandi) ni nchi ya Ulaya kwenye kisiwa cha Bahari ya Atlantiki ya kaskazini. Iko 300 km kutoka Greenland upande wa magharibi na 1000 km kutoka Norway upande wa mashariki. Eneo lake ni 103,000 km² lakini idadi ya watu ni lakhi tatu pekee. Si sehemu ya rasi ya Skandinavia lakini inahesabiwa kati ya nchi za Skandinavia.
Contents |
[edit] Wakazi
Watu wa Iceland karibu wote ni Waskandinavia. Lugha ya Kiiceland bado inafanana sana na ile Kinorway cha kale kilicholetwa kisiwani na wakazi wa kwanza miaka 1000 iliyopita. Watu bado wanaelewea mashairi yaliyotunzwa tangu zamani ile.
Karibu Waiceland wote ni Wakristo Waluteri. Kanisa la Kiluteri ni dini rasmi ya nchi. Kuna pia wakatoliki wachache na wafuasi wachache sana wa imani mbalimbali.
[edit] Historia
Iceland iko mbali na bara za Ulaya na Amerika tena katika mazingira baridi. Inaaminika haikuwa na watu kabisa hadi mwaka 800 BK. Wataalamu hawakubaliani kama ni mabaharia kutoka Norway au Ueire waliobahatika kufika kisiwani na kujenga makao ya kwanza.
Hakika waliofika wengi kidogo walikuwa Waviking au Wanorway wa kale katika karne ya 9 BK. Kama Waeire walikuwepo walifukuzwa au kuwa sehemu za Waviking. Mtu wa kwanza aliyekumbukwa kwa jina alikuwa Flóki Vilgerðarson.
Waviking waliofika walikuja pamoja na familia na watumishi au watumwa wao. Mnamo mwaka 930 BK machifu na wasimamizi wa familia zilizokuwepo walipatana kuhusu aina ya katiba kwa Iceland. Walianzisha bunge ya Althing. Ilikuwa mkutano wa watu 36 walioitwa "Godi" wakiwa na cheo cha kuunganisha madaraka ya chifu, hakimu na kuhani. Utaratibu huu wa kuwa na bunge umeendelea hadi leo bila kusimama. Hivyo Iceland ni nchi ya pekee amabako utaratibu wa kidemokrasia wa kale umeendelea wakati katika nchi za Ulaya nafasi ya wafalme au watawala wengine iliongezeka na kumeza haki zote za watu wa kawaida.
Mwaka 985 Mwiceland aligundua njia ya kufika Greenland na baadaye Amerika ya Kaskazini. Mviking mmoja kwa jina "Erik Mwekundu" alifukuzwa kisiwani kwa sababu alikuwa mwuaji. Alielekea magharibi kwa jahazi yake na kufika kwanza Greenland halafu pwani la Kanada ya leo. Aliita bara jipya "nchi ya mzabibu" kwa sababu alikuta aina ya mizabibu isipokuwa bila matunda.
Tangu 1262 uhuru wa Iceland ilikwisha kwa sababu viongozi walijiunga na Ufalme wa Norway. Iceland iliendelea kuwa na bunge lake na madaraka mbalimbali -hasa kwa sababu usafiri uliendelea kuwa vigumu- lakini mabwana wakuu walikuwa sasa waalme wa Skandinavia, kwanza Wanorway, baadaye Wadenmark.
Mwaka 1918 Denmark ilirudisha madaraka yote ya serikali kwa Waiceland wenyewe isipokuwa mfalme wa Denmark aliendelea kama Mkuu wa nchi.
Wakati wa Vita Kuu ya Dunia ya Pili Denmark ilivamiwa na Ujerumani na Althing iliamua ya kwamba kuanzia sasa kisiwa kitajitawala kabisa. Mwaka 1944 Iceland ilipata uhuru kamili.
Baada ya vita Iceland ilikuwa nchi mwanachama ya NATO lakini haina wanajeshi hadi leo. Ilifanya mkataba na Marekani ya kuwa Waamerika wanapewa haki ya kutumia kituo cha ndege kisiwani na kwa upande mwingine wanaahidi kutetea Iceland.
[edit] Utamaduni
HAdi leo Waiceland hawana majina ya pili au ya familia. Kila mtoto anapewa jina lake la kwanza halafu jina la baba - wakati mwingine pia jina la mama. Kama mto ni wa kiume "-son" (=mwana) itaongezwa, kama ni binti "-dottir" (binti).
Kwa mfano mwimbaji wa kike wa Iceland mashuhuri Björk Guðmundsdóttir alipewa jina la "Björk". Baba yake alikuwa Guðmund hivyo anatumia jina hili pamoja na "-dottir": Guðmundsdottir: "Björk binti wa Guðmund". Kama mwenyewe atamzaa binti anaweza kuitwa "Björkdottir" lakini mara nyingi jina la baba hutumiwa. Wanawake waneendelea na jina hili hawachi wakati wa kuolewa.
[edit] Miji
Reykjavík ni mji mkuu wa Iceland pia bandari kubwa na kitovu cha kiuchumi na kiutamaduni. Miji mingine ni pamoja na Akureyri, Kópavogur, Hafnarfjördhur, Keflavík na Vestmannaeyjar.
[edit] Jiografia
Iceland ina asili ya kivolkeno. Ni kisiwa kikubwa cha safu ya mgongo kati wa Atlantiki mahali ambako mabamba ya Amerika ya Kaskazini na Ulaya-Asia yanakutana. Kwa sababu hii kuna milima mengi hasa volkeno ni nyingi.
Kwa ujumla hali ya hewa ni baridi na barafuto zinafunika sehemu kubwa ya nchi. Hasa nyanda za juu ni baridi mno hakuna mimea. Karibu makazi yote ya watu ni karibu na pwani. Kusini ya kisiwa haikuwa baridi mno kwa sababu ya mkondo wa ghuba linaloendelea kusukuma maji ya ghuba la Mexiko hadi Atlantiki ya kaskazini. Mkondo huu unapofika Iceland si ya moto tena lakini vuguvugu kidogo hivyo inazuia baridi kali sana.
Volkeno zimesababisha kuwepo kwa maji ya moto mahali pengi. Waiceland wanapenda kuogelea nje katika mabwawa hata wakati wa theluji katika maji ya moto kutokana na joto la kivolkeno. Joto hili linatumika kidogo hata kwa kilimo; linapasha moto nyumba za kioo na kuwezesha mimea kuzaa matunda mwaka wote hata wakati wa baridi kali. Kwa njia hii Iceland inavuna ndizi na machungwa yake!