Web - Amazon

We provide Linux to the World


We support WINRAR [What is this] - [Download .exe file(s) for Windows]

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
SITEMAP
Audiobooks by Valerio Di Stefano: Single Download - Complete Download [TAR] [WIM] [ZIP] [RAR] - Alphabetical Download  [TAR] [WIM] [ZIP] [RAR] - Download Instructions

Make a donation: IBAN: IT36M0708677020000000008016 - BIC/SWIFT:  ICRAITRRU60 - VALERIO DI STEFANO or
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Kiswahili - Wikipedia

Kiswahili

From Wikipedia

Maeneo penye wasemaji wa Kiswahili
Maeneo penye wasemaji wa Kiswahili

Kiswahili ni lugha ya kibantu yenye misamiati mingi ya kiarabu inayozungumzwa katika eneo kubwa la Afrika ya Mashariki.

Lugha ilianza takriban miaka 800-1000 iliyopita katika mazingira ya vituo vya biashara vya pwani. Kwa karne nyingi iliandikwa kwa herufi za Kiarabu (سواحلي sawaHili au لغة سواحيلية lugha sawaHiliya). Sarufi ya kwanza pamoja na Kamusi iliandikwa mnamo 1848 na Ludwig Krapf huko Rabai Mpya / Mombasa.

Lugha hii ina utajiri mkubwa wa misamiati na misemo na mithali na mashairi na mafumbo na vitendawili na nyimbo. Nayo inatumika katika mashule kufundishia elimu mbali mbali za dini na dunia, na kuna vitabu vingi vilivyotungwa kwa kutumia lugha hii, vikiwa vya hadithi au hekaya au riwaya.


Tako la kifungu: Historia ya Kiswahili
Tako la kifungu: Lahaja za Kiswahili

Contents

[edit] Wasemaji

Hakuna uhakika kuhusu idadi za wasemaji wa lugha; idadi zinazotajwa zinatofautiana. Wasemaji wa lugha ya kwanza wako labda kati ya milioni 7 hadi 10, na wasemaji wa lugha ya pili zaidi ya milioni sabini. Idadi ya wasemaji wa lugha ya kwanza inakua, kwa sababu lugha inaenea katika maeneo ambapo lugha nyingine zilikuwa lugha kuu, na hasa katika miji ya Tanzania imekuwepo lugha kuu, badala ya lugha za kikabila.

Kati ya nchi ambapo Kiswahili kinatumika ni Tanzania, Kenya, Uganda, Kongo-Kinshasa, Rwanda, Burundi, Msumbiji, Somalia na visiwa vya Bahari Hindi kama Visiwa vya Ngazija (Komoro).

[edit] Lugha rasmi

Kiswahili kimekuwa lugha rasmi katika nchi zifuatazo:

  • Tanzania: Lugha ya taifa; ni lugha ya shule za msingi, lugha ya utawala serikalini na mahakamani; inatumika kote nchini, kanisani, kwenye misikiti, kwa redio, TV na idadi kubwa ya magazeti.
  • Kenya: ni lugha ya taifa lakini Kiingereza ni lugha rasmi ya Kiutawala; Kiswahili ni lugha ya kwanza ya mawasiliano kati ya wanachi wakikutana nje ya eneo penye kabila moja tu; ni lugha inayofundishwa lakini si lugha ya kufundisha mashuleni; ni lugha inayotumika na polisi na jeshi, ni lugha ya kuhutubia wanachi mjini na kitaifa; sehemu za ibada makanisani inatumia Kiswahili; kuna gazeti moja tu ya Kiswahili; sehemu za programu redioni na kwenye TV ni kwa Kiswahili. Lugha inachanganywa mara nyingi na Kiingereza na lugha za maeneo au kikabila.
  • Uganda: imetangazwa kuwa lugha ya kitaifa tangu 2005; iliwahi kuwa lugha ya kitaifa wakati wa utawala wa Idi Amin; wakati wa ukoloni ilifundishwa mashuleni ikaelekea kuwa lugha rasmi pamoja na Kiingereza lakini matumizi haya yalipingwa hasa na Waganda hivyo Waingereza waliacha mipango haya. Ni lugha ya polisi na jeshi hali ambayo imeleta ugumu kwa lugha kukubalika na wanachi wengi kutokana na historia ya utawala wa kijeshi Uganda; watu wengi bado hukumbuka hasa matusi ya wanajeshi waliowatesa wakisema Kiswahili. Lakini kuna maeneo ya Uganda ambako Kiswahili kinatumika na watu wengi kama lugha ya sokoni na barabarani.
  • Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo: Kiswahili ni kati ya lugha nne za kitaifa, pia lugha ya jeshi katika magharibi ya nchi. Kiswahili kimefika na misafara ya biashara ya watumwa na pembe za ndovu kutoka Zanzibar na pwani la Tanganyika. Imeenea zaidi kati ya mchanganyiko wa wafanyakazi kwenye migodi ya Katanga.

[edit] Lugha ya kwanza, lugha ya pili

Kiasili Kiswahili kilikuwa lugha ya kwanza tu ya wakazi wa miji ya Waswahili kwenye pwani, katika sehemu za pwani pia kijijini. Baada ya kuenea kimekuwa lugha ya watu wengi mjini hasa Tanzania lakini pia Kenya.

Kimeenea zaidi kama lugha ya mawasiliano na biashara pale ambako watu wa makabila mbalimbali wanakutana. Pamoja na nchi zinazotajwa hapo juu Kiswahili kinatumika katika Kaskazini ya Msumbiji, Kusini kabisa ya Somalia, Mashariki ya Burundi. Maeneo ya mpaka wa Tanzania kuna pia wasemaji kadhaa huko Malawi na Zambia.

Tanzania na Kenya zilipokea wakimbizi wengi waliojifunza Kiswahili lakini hakuna uhakika kama bado kinatumika wakirudi Rwanda, Sudan au Somalia.

[edit] Kimataifa

Lugha hii leo imekuwa na umuhimu mkubwa duniani kwa jumla, na hasa Afrika, kwa sababu ya kuenea kwake nchi mbali mbali, na kukusanya kwake watu wa makabila na nchi kadha wa kadha wakaweza kufahamiana kwa lugha moja, hasa ilivyokuwa ni lugha mojawapo katika lugha kubwa za Afrika ambazo zinachukuwa mahala pa lugha za kigeni zilizoletwa na Wakoloni, kama Kifaransa, Kiingereza, Kitalia, Kireno na kadhalika.

Leo, imekuwa inatumiwa katika kusambaza habari katika vituo mbali mbali ulimwenguni kama vile Sauti ya Amerika, BBC, Deutsche Welle, Monte Carlo, na nchi nyenginezo za Uchina na Urusi na Irani na kwengineko. Aidha, imekuwa ni mojawapo ya lugha muhimu zinazofundishwa katika vyuo vikuu nchini Marekani, Uingereza, Ulaya, Urusi, Uchina, na barani Afrika.

[edit] Maendeleo ya Kiswahili

Lugha ina maendeleo: inaweza kukua, kukwama au kufa. Athira nyingi hutokea bila mpangilio pale ambako wasemaji wanapokea maneno mapya, wanaacha kutumia maneno mengine au hubadilisha kawaida ya matamshi au sarufi. Haya yote hutokea pia katika uwanja wa Kiswahili.

[edit] Taasisi zinazokuza Kiswahili

Kuna taasisi zinazolenga kukuza na kuimarisha Kiswahili kama vile Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) kwenye chuo kikuu cha Daressalaam pamoja na idara za Kiswahili katika vyuo vikuu vingine vya Kenya na pia Uganda.

Tanzania iko Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Kenya kuna Chama cha Kiswahili cha Taifa (CHAKITA). BAKITA na CHAKITA pamoja na wawakilishi kutoka Uganda wanaandaa kuundwa kwa Baraza la Kiswahili la Afrika Mashariki (BAKAMA).

Uchunguzi wa Kiswahili huendelea pia katika idara za vyuo vikuu vingi duniani.


[edit] Kamusi za Kiswahili

tazama makala ya pekee Kamusi za Kiswahili

Kati ya shughuli muhimu ni kazi ya kukuza msamiati wa Kiswahili yaani kutafuta maneno mapya au kupanusha matumizi ya maneno yaliyopo ili kutaja mambo ya maisha ya kisasa yaliyobadilika. Kutunga kwa kamusi za Kiswahili hupanusha elimu hiyo.


[edit] Marejeo

  • Ashton, E. O. 1944. Swahili Grammar (Including Intonation). London: Longmans.
  • Hinnebusch, T. J. 1979. "Swahili". Katika: T. Shopen (mhariri) Languages and Their Status, uk. 209-293. Cambridge, Massachusetts: Winthrop.
  • Hinnebusch, T. J., and S. M. Mirza. 1979. Kiswahili: Msingi wa Kusema, Kusoma na Kuandika. Lanham, MD: University Press of America.
  • Nurse, D. and Hinnebusch, T. J. 1993. Swahili and Sabaki: A Linguistic History. Berkeley and Los Angeles: University of California Press.
  • Wald, B. 1987. "Swahili and the Bantu Languages". Katika: B. Comrie (mhariri) The World's Major Languages, uk. 991-1014. New York: Oxford University Press.
  • Whiteley, W. 1969. Swahili: The Rise of a National Language. London: Methuen.
  • Zawawi, S. 1971. Kiswahili Kwa Kitendo: An Introductory Course. New York: Harper & Row.


[edit] Viungo vya nje

Our "Network":

Project Gutenberg
https://gutenberg.classicistranieri.com

Encyclopaedia Britannica 1911
https://encyclopaediabritannica.classicistranieri.com

Librivox Audiobooks
https://librivox.classicistranieri.com

Linux Distributions
https://old.classicistranieri.com

Magnatune (MP3 Music)
https://magnatune.classicistranieri.com

Static Wikipedia (June 2008)
https://wikipedia.classicistranieri.com

Static Wikipedia (March 2008)
https://wikipedia2007.classicistranieri.com/mar2008/

Static Wikipedia (2007)
https://wikipedia2007.classicistranieri.com

Static Wikipedia (2006)
https://wikipedia2006.classicistranieri.com

Liber Liber
https://liberliber.classicistranieri.com

ZIM Files for Kiwix
https://zim.classicistranieri.com


Other Websites:

Bach - Goldberg Variations
https://www.goldbergvariations.org

Lazarillo de Tormes
https://www.lazarillodetormes.org

Madame Bovary
https://www.madamebovary.org

Il Fu Mattia Pascal
https://www.mattiapascal.it

The Voice in the Desert
https://www.thevoiceinthedesert.org

Confessione d'un amore fascista
https://www.amorefascista.it

Malinverno
https://www.malinverno.org

Debito formativo
https://www.debitoformativo.it

Adina Spire
https://www.adinaspire.com