Uturuki
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: Kituruki: Yurtta Sulh, Cihanda Sulh ("Amani nyumbani, amani duniani") |
|||||
Wimbo wa taifa: İstiklâl Marşı | |||||
Mji mkuu | Ankara |
||||
Mji mkubwa nchini | Istanbul | ||||
Lugha rasmi | Turkish | ||||
Serikali
Rais
|
Republic Ahmet Necdet Sezer |
||||
National Days Kutangaza Jamhuri |
29 Oktoba 1923 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
780,580 km² (ya 36) 1.3 |
||||
Idadi ya watu - 2005 kadirio - 2000 sensa - Msongamano wa watu |
73,193,000 (ya 17 1) 67,844,903 90/km² (ya 82 1) |
||||
Fedha | Lira Mpya2 (TRY ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
EET (UTC+2) CEST (UTC+3) |
||||
Intaneti TLD | .tr | ||||
Kodi ya simu | +90 |
Uturuki ni nchi ya Asia ya magharibi lakini sehemu ndogo ya eneo lake magharibi ya Bosporus iko Ulaya. Sehemu kubwa ya mipaka yake ni bahari: Mediteranea upande wa magharibi na kusini na Bahari Nyeusi upande wa kaskazini. Kwenye nchi kavi imepakana na Ugiriki na Bulgaria upande wa magharibi, Kaskazini-mashariki na Georgia, Armenia na Azerbaijan, kwa upande wa mashariki na Iran na upande wa kusini na Iraq na Syria.
Jamhuri ya Uturuki ilianzishwa mwaka 1923 na jenerali Kemal Atatürk baada ya vita mbili. Vita ya kwanza ilikuwa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia iliyovunja Dola la Uturuki, na vita ya pili ilifuata wa kuondoa wanajeshi wa Ugiriki na nchi nyingine zilizowahi kuingia ndani sehemu niliyokuwa imebaki baada ya kuvinjika kwa dola kubwa.
Atatürk alileta mabadiliko mengi yaliyolenga kuondoa utamaduni wa kale wa Dola la Uturuki na enzi za utwala wa sultani ya Kiislamu. Magharibi ya nchi imeendelea sana lakini katika maeneo ya mashariki yamebaki nyuma. Siku hizi Uturuki inalenga kuingia katika Umoja wa Ulaya.
Uturuki ina wakazi milioni 69.
Serikali ina utaratibu wa kidemokrasia ya vyama vingi. Utawala ya nchi ni kwa mikoa 81. Mji mkuu ni Ankara katika kitovu cha Anatolia. Mji mkubwa ni Istanbul iliyoitwa zamani Konstantinopoli na zamani zaidi Bizantium iliyokuwa mji mkuu wa Dola la Uturuki hadi 1923.