Web - Amazon

We provide Linux to the World


We support WINRAR [What is this] - [Download .exe file(s) for Windows]

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
SITEMAP
Audiobooks by Valerio Di Stefano: Single Download - Complete Download [TAR] [WIM] [ZIP] [RAR] - Alphabetical Download  [TAR] [WIM] [ZIP] [RAR] - Download Instructions

Make a donation: IBAN: IT36M0708677020000000008016 - BIC/SWIFT:  ICRAITRRU60 - VALERIO DI STEFANO or
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Andorra - Wikipedia

Andorra

From Wikipedia

Principat d'Andorra
Utemi wa Andorra
Flag of Andorra Nembo ya Andorra
Bendera Nembo
Wito la taifa: Virtus Unita Fortior
(Kilatini: "Tabia nzuri ya pamoja ina nguvu zaidi")
Wimbo wa taifa: El Gran Carlemany, Mon Pare
(Kikatalani: "Karolo Mkuu baba yangu"
Lokeshen ya Andorra
Mji mkuu Andorra la Vella
42°30′ N 1°31′ E
Mji mkubwa nchini Andorra la Vella
Lugha rasmi Kikatalani
Serikali
Mtemi Mfaransa
Mtemi Askofu
Rais wa Halmashauri
Bunge - Utemi wa pamoja
{{{leader_names}}}
Uhuru
Paréage
1278
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
468 km² (ya 193)
--
Idadi ya watu
 - 2006 kadirio
 - 2004 sensa
 - Msongamano wa watu
 
67,313 (ya 202)
69,150
152/km² (ya 69)
Fedha Euro (€) (EUR)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET (UTC+1)
CEST (UTC+2)
Intaneti TLD .ad[1]
Kodi ya simu +376
Ramani ya Andorra
Ramani ya Andorra

Utemi wa Andorra (Kikatalani: Principat d'Andorra, Kifaransa: Principauté d'Andorre) ni nchi ndogo katika Ulaya ya kusini magharibi. Iadi ya wakazi ni 70,000. Katiba yake ni ya utemi lakini kuna watemi wawili walioko nje ya nchi. Mmoja ni rais wa Ufaransa na mwingine ni askofu wa Urgell katika Hispania.

Eneo la Andorra ni bonde katika milima ya Pirenei kati ya Hispania na Ufaransa. Mahali pake mlimani palisababisha imeendelea kama nchi ya pekee kwa sababu zamani hapakuwa na njia wala mawasiliano.

Siku hizi imekuwa nchi tajiri kutokana na utalii.

Andorra ni nchi mwanachama ya Baraza la Ulaya lakini si ya Umoja wa Ulaya. Hivyo si sehemu ya eneo la kodi za pamoja la Ulaya. Hali hii inavuta watalii kwa sababu bidhaa nyingi zinapatikana bila kodi kwa bei nafuu kuliko Hispania au Ufaransa; kodi ya ongezeko la thamani (VAT) iko kwenye 4% pekee.

Andorra inatumia pesa ya Euro bila kushiriki katika mkataba wa Euro.

[edit] Historia

Asili ya Andorra kama nchi ya pekee ni katika karne ya 12 na katika mahali pake mlimani na mpakani kati ya Ufaransa na Hispania. Bonde la Andorra ilikuwa chini ya mtemi wa Urgell. Wakati ule hapakuwa bado na himaya moja ndani ya Hispania. Kama historia ingeendelea kama kawaida leo hii Andorra ingekuwa tu sehemu ya wilaya ndani ya Hispania. Lakini katika karne ya 11 palitokea ugomvi kati ya mtemi wa Urgell na jirani yake. Majirani walipatana ya kwamba watatawala bonde kwa pamoja.

Baadaye eneo la jirani liliingizwa katika ufalme wa Ufaransa na haki za kuwa mtemi wa kushirikani ilirithiwa na mfalme wa Ufaransa. Haki za mtemi wa Urgell zilirithiwa na askofu wa Urgell. Katika mwendo wa historia wafalme wa Ufaransa walipotea na rais wa jamhuri ya Ufaransa alirithi haki za utawala kama mtemi wa kushirikiana. Cheo cha askofu wa Urgell imeendelea hadi wakati huu.

Miaka yote ya nyuma Andorra ilikuwa bonde maskini tu bila barabara nzuri hivyo wala Hispania wala Ufaransa iliona umuhimu wa kujitahidi ili upate utawala kamili.

Katika hali hii Andorra imefika katika karne ya 21 ila tu mawasiliano ya kisasa yameondoa upweke na utalii umetajirisha nchi na wakazi wake.

14 Machi 1993 Andorra ilipata katiba iliyoifanya kuwa nchi huru ya kujitegemea kabisa. Nafasi ya watemi wa pamoja ni ya heshima tu na utawala uko mkononi mwa serikali inayochaguliwa na bunge. Tangu 1993 Andorra ni nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa.


Image:WikiLettreMini.png Makala hiyo kuhusu "Andorra" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Andorra kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.


Nchi na maeneo ya Ulaya
Albania | Andorra | Austria | Belarus | Bosnia na Herzegovina | Bulgaria | Kroatia | Denmark | Estonia | Ufaransa | Hungaria | Iceland | Ireland | Italia | Latvia | Liechtenstein | Lithuania | Luxemburg | Masedonia | Malta | Moldova | Monako | Norway | Poland | Romania | San Marino | Serbia na Montenegro3 | Slovakia | Slovenia | Hispania | Ubelgiji | Uceki | Ufini | Ugiriki | Ujerumani | Uholanzi | Ureno | Urusi1 | Uswidi | Uswisi | Ukraine | Uingereza | Vatikan

Maeneo ya Ulaya ya kujitawala chini ya nchi nyingine: Visiwa vya Faroe | Gibraltar | Guernsey | Jan Mayen | Jersey | Isle of Man | Svalbard

Nchi za Asia ambazo ni mwanachama wa baraza la Ulaya au vyombo vingine vya Ulaya: Armenia2 | Azerbaijan1 || Cyprus2 | Georgia1 | Kazakhstan1 | Uturuki1

Nchi zisizokubaliwa na umma wa kimataifa: Abkhazia | Nagorno-Karabakh2 | Ossetia ya Kusini | Transnistria | Jamhuri ya Kituruki ya Cyprus ya Kaskazini2

Maelezo: (1) nchi ya kimabara katika Asia na Ulaya; (2) nchi katika eneo la Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) lakini kiutamaduni huhesabiwa kuwa sehemu ya Ulaya; (3) Inaelekea kugawiwa kuwa nchi mbili za Serbia na Montenegro

Our "Network":

Project Gutenberg
https://gutenberg.classicistranieri.com

Encyclopaedia Britannica 1911
https://encyclopaediabritannica.classicistranieri.com

Librivox Audiobooks
https://librivox.classicistranieri.com

Linux Distributions
https://old.classicistranieri.com

Magnatune (MP3 Music)
https://magnatune.classicistranieri.com

Static Wikipedia (June 2008)
https://wikipedia.classicistranieri.com

Static Wikipedia (March 2008)
https://wikipedia2007.classicistranieri.com/mar2008/

Static Wikipedia (2007)
https://wikipedia2007.classicistranieri.com

Static Wikipedia (2006)
https://wikipedia2006.classicistranieri.com

Liber Liber
https://liberliber.classicistranieri.com

ZIM Files for Kiwix
https://zim.classicistranieri.com


Other Websites:

Bach - Goldberg Variations
https://www.goldbergvariations.org

Lazarillo de Tormes
https://www.lazarillodetormes.org

Madame Bovary
https://www.madamebovary.org

Il Fu Mattia Pascal
https://www.mattiapascal.it

The Voice in the Desert
https://www.thevoiceinthedesert.org

Confessione d'un amore fascista
https://www.amorefascista.it

Malinverno
https://www.malinverno.org

Debito formativo
https://www.debitoformativo.it

Adina Spire
https://www.adinaspire.com