Ureno
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: (hakuna) | |||||
Wimbo wa taifa: A Portuguesa | |||||
Mji mkuu | Lisbon (Lisboa) |
||||
Mji mkubwa nchini | Lisbon | ||||
Lugha rasmi | Kireno1 | ||||
Serikali
Rais
|
Jamhuri Aníbal Cavaco Silva |
||||
Formation Uhuru |
24. Juni 1128 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
92,391 km² (ya 111th) 0.5% |
||||
Idadi ya watu - July 2005 kadirio - 2001 sensa - Msongamano wa watu |
10,495,000 (ya 76) 10,148,259 114/km² (ya 66th) |
||||
Fedha | Euro (€)2 (EUR ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
WET3 (UTC) EST (UTC+1) |
||||
Intaneti TLD | .pt | ||||
Kodi ya simu | +351 |
||||
1Kimiranda imetambuliwa kama lugha rasmi katika eneo ndogo la Ureno ya kaskazini (sheria N.º 7/99). 2Hadi 1999: Escudo ya Ureno 3Azori: UTC-1; UTC in summer |
Ureno (Portugal) ni nchi pembe ya kusini magharibi kabisa ya Ulaya. Upande wa magharibi na kusini imepakana na Bahari ya Atlantiki, na upande wa mashariki na mashariki imepakana na Hispania.
Funguvisiwa vya Atlantiki ni pia sehemu za Ureno. Visiwa hivi ni Azori na Visiwa vya Madeira vilivyoko katika sehemu ya Afrika ya Atlantiki.
Jina la nchi katika Kiswahili limetokana na neno la Kireno "reino" linalomaanisha "ufalme". Wasafiri na wapelelezi Wareno kama Vasco da Gama walijitambulisha kama wawakilishi wa "Reino de Portugale" (ufalme wa Ureno). Ni sehemu ya kwanza tu iliyoingia katika lugha ya Kiswahili.
[edit] Historia
Katika karne KK Ureno ilikaliwa na makabila yale yale ya Kikelti kama Hispania. Waroma walitaja eneo lote la Ureno na Hispania ya leo kwa jina la "Iberia". Tangu mwaka 450 KK sehemu za nchi zilitawaliwa na Wafinisia wa Karthago na yote ikawa baada ya mwaka 200 KK sehemu ya Dola la Roma. Baada ya kuporomoka ya Dola la Roma mnamo 470 BK makabila ya wahamiaji wa Kigermanik walikuwa mabwana wa eneo.
Tangu mwaka 711 Waarabu walivamia nchi na kuitawala. Vita ya kuwaondoa tena iliendelea kwa karne kadhaa. Tangu mwaka 1143 mtawala wa eneo la mji wa Kale katika kaskazini alikuwa na uwezo wa kutosha kujitetea dhidi ya Waarabu na pia dhidi ya majirani katika eneo la Kihispania. Baada ya ushindi katika vita dhidi ya Wahispania mwaka 1128 Afonso I alijitangaza kuwa mtawala wa kujitegemea na baadaye alichukua cheo cha mfalme. Alitumia jina la mji Kale iliyojulikana kama "Porto Kale" (bandari ya Kale) iliyokuwa "Portokale" na baadaye "Portogale".
Nchi hii ndogo ilifaulu kutunza uhuru wake hata baada ya maeneo yote mengine ya jirani kuunganishwa katika ufalme mpya wa Hispania.
Nchi hii ndogo ilikuwa kati ya nchi muhimu zaidi duniani kwa karne mbili za 15 na 16 BK. Wafalme wake walilenga jitihada na nguvu za nchi kwa teknolojia za usafiri baharini. Wareno waliweza kuboresha jahazi zao hadi kupita nchi zote za dunia kwa muda wakafaulu kwenda mbali. Wareno waligundua njia ya kuvuka rasi ya Afrika Kusini na kufika kwenye mabandari ya Afrika ya Mashariki hata Bara Hindi. Ureno ilitajirika kutokana na biashara kati ya India, Asia na Ulaya. Wareno walijenga vituo kama vile boma za Msumbiji na Mombasa wakiwa mabwana wa pwani la Afrika ya Mashariki. Lakini nguvu za nchi ndogo hazikuweza kutetea haya yote. Baada ya kufika kwa mataifa mengine kama vile Uturuki, Uholanzi, Uingereza na Ufaransa Wareno walipaswa kuwaachia maeneo mengi.
Kati ya koloni za Ureno zilibaki hasa Msumbiji, Angola, Guinea ya Ikweta, São Tomé na Príncipe katika Afrika, Brazil katika Amerika ya Kusini (hadi 1822) pamoja na maeneo madogomadogo kama Goa kwenye Bara Hindi, Timor ya Mashariki katika funguvisiwa ya Indonesia, mji wa Makao katika Uchina.
Mwaka 1910 Ureno iliona mapinduzi ikawa jamhuri. Tangu 1926 hadi 1974 ilikuwa na serikali za kidikteta. Baada ya mapinduzi ya 1974 Ureno iliacha koloni zake zilizobaki isipokuwa Makao kwa sababu Uchina haukuwa tayari kuipokea hadi 1999.
Ureno ikajiunga na Umoja wa Ulaya mwaka 1986 ikaona maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Nchi na maeneo ya Ulaya | |
---|---|
Albania | Andorra | Austria | Belarus | Bosnia na Herzegovina | Bulgaria | Kroatia | Denmark | Estonia | Ufaransa | Hungaria | Iceland | Ireland | Italia | Latvia | Liechtenstein | Lithuania | Luxemburg | Masedonia | Malta | Moldova | Monako | Norway | Poland | Romania | San Marino | Serbia na Montenegro3 | Slovakia | Slovenia | Hispania | Ubelgiji | Uceki | Ufini | Ugiriki | Ujerumani | Uholanzi | Ureno | Urusi1 | Uswidi | Uswisi | Ukraine | Uingereza | Vatikan
Maeneo ya Ulaya ya kujitawala chini ya nchi nyingine: Visiwa vya Faroe | Gibraltar | Guernsey | Jan Mayen | Jersey | Isle of Man | Svalbard Nchi za Asia ambazo ni mwanachama wa baraza la Ulaya au vyombo vingine vya Ulaya: Armenia2 | Azerbaijan1 || Cyprus2 | Georgia1 | Kazakhstan1 | Uturuki1 Nchi zisizokubaliwa na umma wa kimataifa: Abkhazia | Nagorno-Karabakh2 | Ossetia ya Kusini | Transnistria | Jamhuri ya Kituruki ya Cyprus ya Kaskazini2 Maelezo: (1) nchi ya kimabara katika Asia na Ulaya; (2) nchi katika eneo la Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) lakini kiutamaduni huhesabiwa kuwa sehemu ya Ulaya; (3) Inaelekea kugawiwa kuwa nchi mbili za Serbia na Montenegro |