Liechtenstein
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: none | |||||
Wimbo wa taifa: Oben am jungen Rhein ("Juu ya Rhine changa") |
|||||
Mji mkuu | Vaduz |
||||
Mji mkubwa nchini | Schaan | ||||
Lugha rasmi | Kijerumani | ||||
Serikali
Mtemi wa Liechtenstein
Regent Mkuu wa serikali |
Ufalme wa kikatiba (Utemi) Hans-Adam II wa Liechtenstein Alois wa Liechtenstein Otmar Hasler |
||||
Uhuru Tarehe |
1806 (Mkataba wa Pressburg) | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
160 km² (ya 215) negligible |
||||
Idadi ya watu - Julai 2006 kadirio - 2000 sensa - Msongamano wa watu |
33 987 (ya 211) 33,307 210/km² (ya 5) |
||||
Fedha | Frank ya Uswisi (CHF ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) |
||||
Intaneti TLD | .li | ||||
Kodi ya simu | +{{{calling_code}}} |
Utemi wa Liechtenstein (Kijerumani: Fürstentum Liechtenstein) ni nchi ndogo katika Ulaya ya Kati. Imepakana na Uswisi na Austria. Ni kati ya nchi ndogo nne duniani. Mji mkuu ni Vaduz wanapoishi wakazi 5000.
Contents |
[edit] Jiografia
Nchi yote ina urefu wa 24.56 km kutoka kaskazini hadi kusini na upana hadi 12.36 km. Urefu huu unafuata mwendo wa Rhine ambayo ni mto wa pekee nchini pia ni mpaka na Uswisi. Upande wa mashariki na karibu na mpaka wa Austria milima hupanda hadi kimo cha 2,599 m.
[edit] Uchumi
Lichtenstein imekuwa nchi tajiri baada ya vita kuu ya pili ya dunia kwa sababu serikali ya mtemi ilidai kodi za duni kabisa zilizohamasisha makampuni mengi ya nje kuunda ofisi zao nchini. Kuna pia benki nyingi zinazosemekana zinaficha pesa za matajiri ambao wangetakiwa kulipa kodi ya mapata nyumbani kwao.
[edit] Siasa
Mkuu wa nchi ni mtemi Hans-Adam II anayeitwa kwa jina kamili "Johannes „Hans“ Adam II. Ferdinand Alois Josef Maria Marko d'Aviano Pius von und zu Liechtenstein". Tangu 15 Agosti 2004 amemkabidhi mwanawe Alois madaraka ya utawala.
Bunge ya wabunge 25 huchaguliwa na wananchi wote. Sheria zote zinapaswa kukubaliwa na mtemi. Waziri watano wa serikali huteuliwa na bunge na kuthebitishwa na mtemi. Wananchi wote wana haki ya kupeleka mapendekezo ya sheria, au kudai kura ya wananchi wote juu ya sheria iliyopitishwa na bunge na kutehbitishwa na mtemi.
[edit] Michezo
Tangu 1984 Liechtenstein imejiunga na FIFA na UEFA na inashiriki tangu 1994 katika uteuzi wa timu za soka katika mashindano ya kombe la Ulaya na kombe la dunia.
Hata kama nchi ya wakazi 33,000 haina klabu mashuhuri Waliechtensetin waliweza kushtusha wapinzani wao mara kadhaa.
1996 klabu ya Vaduz ilishinda klabu ya Latvia FC Universitate Riga 1–1 na 4–2 lakini ilishindwa baadaye na Paris St Germain.
Timu ya kitaifa ya 2004 iliweza kumalizana na Ureno 2–2 na kushinda Luxemburg 4-0.
Nchi na maeneo ya Ulaya | |
---|---|
Albania | Andorra | Austria | Belarus | Bosnia na Herzegovina | Bulgaria | Kroatia | Denmark | Estonia | Ufaransa | Hungaria | Iceland | Ireland | Italia | Latvia | Liechtenstein | Lithuania | Luxemburg | Masedonia | Malta | Moldova | Monako | Norway | Poland | Romania | San Marino | Serbia na Montenegro3 | Slovakia | Slovenia | Hispania | Ubelgiji | Uceki | Ufini | Ugiriki | Ujerumani | Uholanzi | Ureno | Urusi1 | Uswidi | Uswisi | Ukraine | Uingereza | Vatikan
Maeneo ya Ulaya ya kujitawala chini ya nchi nyingine: Visiwa vya Faroe | Gibraltar | Guernsey | Jan Mayen | Jersey | Isle of Man | Svalbard Nchi za Asia ambazo ni mwanachama wa baraza la Ulaya au vyombo vingine vya Ulaya: Armenia2 | Azerbaijan1 || Cyprus2 | Georgia1 | Kazakhstan1 | Uturuki1 Nchi zisizokubaliwa na umma wa kimataifa: Abkhazia | Nagorno-Karabakh2 | Ossetia ya Kusini | Transnistria | Jamhuri ya Kituruki ya Cyprus ya Kaskazini2 Maelezo: (1) nchi ya kimabara katika Asia na Ulaya; (2) nchi katika eneo la Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) lakini kiutamaduni huhesabiwa kuwa sehemu ya Ulaya; (3) Inaelekea kugawiwa kuwa nchi mbili za Serbia na Montenegro |