Sahara ya Magharibi
From Wikipedia
Sahara ya Magharibi ni eneo kwenye mwambao wa Afrika ya Kaskazini-Magharibi. Imepakana na Moroko upande wa Kaskazini, Algeria upande wa mashariki na Mauretania upande wa kusini, halafu Bahari Atlantiki upande wa magharibi.
Ilitangazwa nchi huru mwaka 1976 kama Jamhuri ya Sahara ya Kidemokrasia ya Kiarabu lakini inatawaliwa na Moroko kama mikoa yake ya kusini. Nchi nyingi za dunia pamoja na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika hazitambui kuwa Sahara Magharibi ni sehemu ya Moroko. Nchi 53 zinaikubali kama Jamhuri. Hali halisi sehemu kubwa ya ardhi yake inatawaliwa na Moroko inayodai ni sehemu ya eneo lake la kitaifa. Sehemu kubwa ya wananchi asilia wako nje ya eneo kama wakimbizi katika makambi makubwa nchini Algeria.
Contents |
[edit] Historia
[edit] Kabla ya ukoloni
Sahara ya Magharibi haikuwahi kuwa na dola la pekee katika historia yake. Wakazi wake walikuwa makabila ya Waberber waliochanganyika na Waarabu tangu uvamizi wa Kiislamu. Wakazi walikuwa wachache kwa sababu eneo lote ni jangwa. Kuna kilimo kidogo tu katika oasisi. Ni eneo la asili la Wamurabitun waliojenga utawala juu ya Moroko, Hispania na sehemu kubwa ya Afrika ya Kaskazini hadi mipaka ya Misri na Senegal mnamo karne ya 11 BK.
[edit] Koloni ya Hispania
1884 Hispania ilichukua utawala wa maeneo ya pwani na kutangaza koloni yake iliyokuwa "Sahara ya Hispania". Ilivutwa hasa na malighafi za fosfeti. Tangu 1973 harakati ya kupambania uhuru ya Polisario ilipigana na jeshi la Wahispania. Wakati uleule dikteta ya Hispania Francisco Franco aligonjeka kabla ya kifo chake. Serikali yake ilianza majadiliano na POLISARIO kuhusu uhuru lakini majirani ya Moroko na Mauretania walidai ya kwamba koloni ya Hispania ingestahili kuwa sehemu ya maeneo yao.
Maroko iliomba usaidizi wa Mahakama ya Kimataifa yalioamua tar. 16.10.1975 ya kwamba hakuna haki za Moroko juu ya Sahara ya Magharibi na azimio lolote kuhusu hali ya eneo linapaswa kuamuliwa na wenyeji wenyewe. Wakati huohuo tume la Umoja wa Mataifa lilitembelea Sahara ya Magharibi likatoa taarifa ya kwamba wananchi wlitaka uhuru.
Mfalme Hassan II wa Moroko aliongeza shindikizo Novemba 1976 kwa kutuma wananchi Wamoroko 350.000 wasio na silaha mpakani waliovuka mpaka kidogo wakati wanajeshi Wahispania hawakufyatulia risasi. Baada ya kifo cha Franco siku chache baadaye Wahispania waliamua kuondoka katika matatizo haya. Walifanya mapatano na Maroko na Mauretania bila kushauriana na wananchi wenyewe ili Maroko ichukue sehemu ya kaskazini na Mauretania sehemu ya kusini ya koloni. Disemba 1975 Wahispania waliondoka. Wanajeshi Wamaroko walingia na Polisario ilitangaza Jamhuri ya Sahara ya Kidemokrasia ya Kiarabu mwanzo wa 1976.
[edit] Polisario ilipigania uhuru
Hii ilikuwa mwanzo wa vita ya miaka mingi. Polisario ilishambulia wavamizi waliokuwa na nguvu tofauti: jeshi hafifu la Mauretania na jeshi lenye nguvu na silaha za kisasa la Moroko. Idadi kubwa ya wananchi walikimbia wakapewa makambi katika Algeria ya kusini walipoweza kujitawala. Algeria ilikubali Jamhuri ya Sahara na kuwaruhusu Polisario kutumia makambi kama vituo vya kijeshi dhidi ya Moroko.
Polisarion ilifaulu kushinda jeshi la Mauretania hata walishambulia mji mkuu wa Nuakshott. Waarabu wengi wa Mauretania waliunga mkono na wenzao wa Sahara ya Magharibi. 1979 Mauretania iliondoka kabisa katika Sahara ya Magharibi. Lakini sasa Wamoroko waliingia na kuteka eneo lote.
Vita ilikuwa vigumu kwa sababu Polisario haikuwa na uwezo wa kushinda jeshi lenye silaha za kisasa kabisa lakini Wamoroko walishindwa vilevile kuwazuia Polisario wasiingie mara kwa mara na kupita makambi ya jeshi la Moroko na kushambulia vituo vyao kwa vikundi vidogo. Moroko ilianza kujenga ukuta na vizuizi jangwani kwa urefu wa 2,720 km inayoacha sehemu ndogo ya jagnwa mkononi wa Polisario na sehemu penye vijiji na miji mkonono wa Moroko.
[edit] Eneo lililogawiwa
Vita imepunzika tangu 1991 kufuatana na mapatano kati ya Moroko, Polisario na Umoja wa Mataifa. Kura ya wananchi kuhusu swali la Uhuru ilipataniwa. Kura hii ilitakiwa kufanyiwa 1992 lakini imeshindikana hadi leo kwa sababu Moroko na Polisario hawakubaliani ni nani mwenye haki ya kupiga kura. Polisario ilikataa wakazi wengi waliohamia kutoka Moroko wasipige kura; Moroko ilitia wasiwasi ya kwamba wakazi wengi wa makambi huko algeria si wenyeji asilia ya Sahara ya Magharibi hivyo wasipige kura.
Maroko imeendelea kupeleka raia zake ili wajenge nyumba katika Sahara ya Magharibi. Idadi yao imeshapita idadi ya wenyeji asilia waliobaki ndani ya maeneo chini ya Moroko.
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad |Cote d'Ivoire | Djibouti | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia |