Web - Amazon

We provide Linux to the World


We support WINRAR [What is this] - [Download .exe file(s) for Windows]

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
SITEMAP
Audiobooks by Valerio Di Stefano: Single Download - Complete Download [TAR] [WIM] [ZIP] [RAR] - Alphabetical Download  [TAR] [WIM] [ZIP] [RAR] - Download Instructions

Make a donation: IBAN: IT36M0708677020000000008016 - BIC/SWIFT:  ICRAITRRU60 - VALERIO DI STEFANO or
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Mali - Wikipedia

Mali

From Wikipedia


Republique du Mali

Jamhuri ya Mali
Flag of Mali Nembo ya Mali
Bendera Nembo
Wito la taifa: Taifa moja, Lengo moja, Imani moja (Kifaransa: Un peuple, un but, une foi)
Wimbo wa taifa: Pour l'Afrique et pour toi, Mali (Kwa Afrika na kwako Mali)
Lokeshen ya Mali
Mji mkuu Bamako
12°39′ N 8°0′ W
Mji mkubwa nchini Bamako
Lugha rasmi Kifaransa
Serikali
Rais
Waziri Mkuu
Jamhuri ya
Amadou Toumani Touré
Ousmane Issoufi Maïga
Uhuru
Tarehe
kutoka Ufaransa
Septemba 22, 1960
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
1,240,278 km² (ya 24)
1.6%
Idadi ya watu
 - Julai 2005 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
12,291,529 (ya 67)
9/km² (ya 174)
Fedha CFA franc (XOF)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC0)
(UTC+1)
Intaneti TLD .ml
Kodi ya simu +223
Ramani ya Mali
Ramani ya Mali

Mali (République du Mali = Jamhuri ya Mali) ni nchi ya Afrika ya Magharibi. Imepakana na Algeria, Mauretania, Niger, Burkina Faso, Cote d'Ivoire na Senegal. Haina pwani la bahari. Sehemu ya juu ni mlima wa Hombori Tondo (1155 m) iliyoko katikati ya nchi. Kaskazini sehemu kubwa la eneo la Mali ni jangwa la Sahara. Wakazi walio wengi huishi kusini karibu na mito ya Senegal na Niger.

Contents

[edit] Jiografia

Theluthi mbili za eneo la Niger ni jangwa. Maneneo mengine ni ya Sahel na kanda la Sudan. Sehemu za kusini ni hasa tambarare za bonde la mto Niger.

Hali ya hewa ni tofauti kulingana na eneo. Kuna kanda tatu:

  • Kanda la jangwani kaskazini - usimbishaji chini ya 100 mm, yabisi na yabisi sana. Hapa wanaishi wafugaji pekee.
  • Kanda la Sahel: mbuga nusu yabisi inayobadilika kuwa savana kusini penye mvua zaid. Pana kilimo kando la mto Niger.
  • Kanda la Sudan lina usimbishaji wa 1400 mm kwa mwaka. Lina savana ilhali miti inaongezeka hadi kufika hali ya misitu kabisa katika kusini.

Kuna malighafi kama vile dhahabu, urani, fosfati, kaolini, chumvi na chokaa.


[edit] Wakazi, lugha, dini

Katika maeneo makubwa ya kaskazini wanaishi makabila ya Waberber hasa Mauri na Tuareg ambao ni wahamiaji. Ndio 10% ya wakazi wa nchi wakikalia asilimia kubwa ya eneo.

Kikundi kikubwa ndio Wabambara (30%) katika eneo la mji mkuu Bamako, halafu wako Wamalinké, Wapeuls, Wadogon, Wasonghai na wengine.

[edit] Lugha

Kutokana na ukoloni Kifaransa kimekuwa lugha rasmi. Kibambara kinaeleweka na takriban 60% za wakazi.

[edit] Dini

Uislamu ni dini kubwa nchini ya 85-90 % za wakazi. Wakristo Wakatoliki na Waprotestant ni labda 4%, wengine wanafuata dini asilia. Ibada na desturi asilia zinapatikana pia katika mazingira ya Waislamu.


[edit] Historia ya Mali

Mali ina historia ndefu ambayo ni historia ya pamoja ya nchi za kanda la Sahel na kanda la Sudan.

Zamani za Wafinisia na za Waroma palikuwa na mawasiliano ya biashara na nchi za Mediteranea kupitia wanafayabiashara Waberber walioelewa njia za Sahara. Uvamizi wa Wavandali katika Afrika ya Kaskazini ulivuruga mawasiliano haya.

Dola la Ghana
Dola la Ghana

Baada ya uvamizi wa Waarabu na uenezaji wa Uislamu biashara ilianza upya. Ndio Waberber Waislamu walioingiza dini mpya hata kusini ya Sahara.

Katika eneo la Mali ya leo pamoja nchi jirani ni hasa madola matatu makubwa yaliyotawala upande wa kusini wa njia za biashara iliyovuka Sahara.

[edit] Dola la Ghana

Dola la kwanza ilikuwa Dola la Ghana. Kuanzia karne ya 8 BK hadi mwaka 1076 lilitawala biashara ya dhahabu, pembe za ndovu na chumvi. Mji mkuu ulikuwa Kumbi Sale yenye wakazi 30,000 katika Mauretania ya leo. Taarifa za wanahistoria Waarabu zimeonyesha ufalme tajiri. Utamatuni wake haukuwa kiislamu bali kiafrika asilia. Mwisho wake ulianza wakati jeshi la Wamurabitun kutoka Moroko lilivuka jangwa na kuvamia Kumbi Sale.

[edit] Dola la Mali

Eneo la Dola la Mali
Eneo la Dola la Mali

Mali ilianza kama ufalme mdogo wa Wamalinke kando la Ghana. Wakati wa karne ya 13 ilianza kupanuka chini ya mfalme Sundiata Keita. Sundiata alipokea Uislamu mwenyewe mnamo 1240 BK na wafalme baada yake waliendela kuwa Waislamu.

Mfalme wa Mali aliyejulikana zaidi ndiye Mansa Kankan Musa I (1312–37). 1324-25 alihiji kwenda Makka. Alisafiri na dhahabu nyingi sana. Huku Misri alitoa zawadi kiasi cha kuharibu thamani ya dhahabu kwa miaka 12 iliyofuata.

Wakati ule mji wa Timbuktu ulikuwa kitovu cha biashara na elimu iliyojulikana kote katika dunia ya kiislamu hata Ulaya. Katika karne ya 14 BK uwezo na utawala wa Mali ilipungua na Songhai ilichukua nafasi yake.

[edit] Dola la Songhai

Eneo la Dola la Songhai
Eneo la Dola la Songhai

Asili ya Wasonghai ilikuwa Nigeria ya Kaskazini ya leo. Walipanusha utawala wao kuelöekea magharibi wakapokeas Uislamu wakati wa uvamizi wa Almurabitun.

Mnamo 1250 walikuwa chini ya Mali lakini katika karne ya 14 walijipatia uhuru tena wakaanza kushika maeneo ya Mali yenyewe. Kelele ya nguvu yake ilikua wakati wa mfalme Askia Mohammad I katika karne ya 16 walipotawala eneo kubwa kutoka Kano (Nigeria) hadi pwani la Atlantiki. Wakati wake mji wa Timbuktu ilitembelewa na msafiri Leo Africanus aliyeleta baadaye habari za nchi hadi Ulaya.

Utawala wao uliporomoka baada ya mashumbulizi kutoka Moroko 1591. Wakati ule mataifa ya Ulaya yameshaanza kufika kwenye mwambao wa Afrika ya Magharibi wakifungua biashara ya moja kwa moja na Ulaya. Umuhimu wa biahsara ya kuvuka Sahara ulipungua vikali pamoja na faida iliyopatikana kwa watawala katika maeneo ya Sahel.

[edit] Kipindi cha madola madogo na jihadi

Kilichofuata kilikuwa kipindi cha madola madogo. Viongozi Waislamu walijaribu mara kadhaa kujenga utawala juuy a eneo lote. Anyejulikana zaidi alikuwa Alhaj Omar alipiga vita katika jina la dini ya Kiislamu dhidi ya Bambara waliofuata utamaduni na dini za asilia. Mtoto wake Alhaj Omar aliyeitwa Ahmadu alijaribu kuendeleza jihadi yake. Lakini wakati ule Wafaransa walianza kupanuka katika Afrika ya Magharibi wakamshinda.

Mali ikawa koloni ya Ufaransa kuanzia mwaka 1895. Ilikuwa sehemu ya Afrika ya Magharibi ya Kifaransa, kuanzia 1920 ya Sudan ya Kifaransa.

Mji wa Bamako
Mji wa Bamako

[edit] Uhuru

1960 Mali pamoja na Senegal zilipata uhuru kama "Shirikisho la Mali".Baada ya Senegal kuacha umoja huu Jamhuri ya Mali chini ya rais ya kwanza Modibo Keïta ikawa nchi ya kujitegemea.

Keita alipinduliwa 1968 na wanajeshi akishtakiwa ameharibu uchumi na kijitajirisha. Kiongozi mpya Moussa Traoré alitawala kama diketa ya kijeshi, baadaya kwa msada wa katiba ya chama kimoja.

Mabadiliko yaliyotokea kote Afrika tangu mwisho wa Ukomunisti kuanzia miaka ya 1990 yalisababisha kupinduliwa kwa Tarore katika Machi 1991 na kamati ya kijeshi iliyoongozwa na Amadou Toumani Touré.

Katiba mpya ya 1992 iliunda kipindi cha kura huru alimoshinda Amadou.

Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad |Cote d'Ivoire | Djibouti | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia
Our "Network":

Project Gutenberg
https://gutenberg.classicistranieri.com

Encyclopaedia Britannica 1911
https://encyclopaediabritannica.classicistranieri.com

Librivox Audiobooks
https://librivox.classicistranieri.com

Linux Distributions
https://old.classicistranieri.com

Magnatune (MP3 Music)
https://magnatune.classicistranieri.com

Static Wikipedia (June 2008)
https://wikipedia.classicistranieri.com

Static Wikipedia (March 2008)
https://wikipedia2007.classicistranieri.com/mar2008/

Static Wikipedia (2007)
https://wikipedia2007.classicistranieri.com

Static Wikipedia (2006)
https://wikipedia2006.classicistranieri.com

Liber Liber
https://liberliber.classicistranieri.com

ZIM Files for Kiwix
https://zim.classicistranieri.com


Other Websites:

Bach - Goldberg Variations
https://www.goldbergvariations.org

Lazarillo de Tormes
https://www.lazarillodetormes.org

Madame Bovary
https://www.madamebovary.org

Il Fu Mattia Pascal
https://www.mattiapascal.it

The Voice in the Desert
https://www.thevoiceinthedesert.org

Confessione d'un amore fascista
https://www.amorefascista.it

Malinverno
https://www.malinverno.org

Debito formativo
https://www.debitoformativo.it

Adina Spire
https://www.adinaspire.com