Diego Garcia
From Wikipedia
Diego Garcia ni kisiwa cha Kiingereza katika Bahari Hindi. Ni sehemu ya funguvisiwa Chagos. Ni kituo kikubwa cha kijeshi cha Marekani katika Bahari Hindi.
Kati ya 1850 na 1965 kisiwa kilikuwa sehemu ya eneo la Mauritius. Mwaka 1971 Uingereza ilikodi Diego Gracia kwa jeshi la Marekani. Waamerika walitaka kuwa na kituo cha kijeshi katika mashindano yao na Urusi.
Katika miaka miwili iliyofuata wenyeji wote wa funguvisiwa waliondolewa visiwani leo vyote ni chini ya jeshi la Marekani. Waliohamishwa na watoto wao wanaishi leo huko Mauritius, Shelisheli na Uingereza. Wengi wao wanapigania haki ya kurudi. Mahakama ya Uingereza iliwaruhusu mwaka 2000 warudi tena lakini serikali imekataa mwaka 2004.
Diego Garcia ilikuwa kituo muhimu katika vita za Marekani huko Afghanistan na Irak. Ndege za kijeshi za aina B-52 zinatoka hapa pamoja na ndege za kubeba petroli.
Marekani ina pia kituo cha meli za kijeshi kisiwani.
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad |Cote d'Ivoire | Djibouti | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia |