Web - Amazon

We provide Linux to the World


We support WINRAR [What is this] - [Download .exe file(s) for Windows]

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
SITEMAP
Audiobooks by Valerio Di Stefano: Single Download - Complete Download [TAR] [WIM] [ZIP] [RAR] - Alphabetical Download  [TAR] [WIM] [ZIP] [RAR] - Download Instructions

Make a donation: IBAN: IT36M0708677020000000008016 - BIC/SWIFT:  ICRAITRRU60 - VALERIO DI STEFANO or
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Réunion - Wikipedia

Réunion

From Wikipedia

Région Réunion
Image:france_flag_medium.png Image:Blason ile reunion 1925.jpg
Jina la Kifaransa Région Réunion
Jina la kawaida Reunion
Mji Mkuu Saint-Denis
Eneo 2,512 km²
Mkuu wa Mkoa Paul Vergès
(PCR) (tangu 1998)
Idadi ya wakazi 706,300
Sensa ya mwaka 1999
Wakazi kwa km² 309
Wilaya (arrondissements) 4
Ramani Reunion na Ufaransa bara


Réunion (Kifaransa: La Réunion) ni kisiwa cha Kiafrika na mkoa wa ng'ambo wa Ufaransa (Kifaransa: département d'outre-mer, au DOM) katika Bahari Hindi upande wa mashariki wa Madagaska. Kisheria hali yake ni sawa na mikoa mingine ya Ufaransa hivyo ni pia sehemu ya Umoja wa Ulaya.

Contents

[edit] Eneo lake

Reunion iko 800 km upande wa mashariki wa Madagaska. Pamoja na visiwa vya Mauritius na Rodrigues ni sehemu ya visiwa vya Maskareni. Kisiwa kina eneo la 2.512 km² kikiwa na upenyo wa 50 hadi 70 km. Milima mikubwa ni ya kivolkeno. Upande wa mashariki wa kisiwa ndipo mlima wa "Piton de la Fournaise" mwenye 2611 m uliolipuka zaidi ya mara 100 tangu kumbukumbu ya kimaandishi ilianzishwa mwaka 1640. Mlipuko wa mwisho hadi leo ilikuwa tar. 4.10.2005. Mlima wa "Piton des Neiges" ndio mkubwa kisiwani ikiwa na 3070 m juu ya UB.

[edit] Hali ya hewa

Hali ya hewa ni ya joto mwaka wote. Majira ya mvua ndiyo kati ya Disemba hadi Machi.

[edit] Historia na Utawala

Taarifa za kwanza za kimaandishi hudokeza ya kwamba kisiwa ilikuwa bila wakazi. Waarabu waliita "dina margabin" yaani kisiwa cha magharibi. Mbaharia Mreno Diego Dias alifika tar. 9.02.1513 ambayo ni sikukuu ya Mt. Apolonia katika desturi ya kikatoliki na kukiita kisiwa kwa jina la mtakatifu huyu "Santa Apolonia" jinsi inavyoonekana katika ramani za kwanza. Baadaye Wareno walitumia jina la nahodha maarufu Pedro de Mascarenhas na kujumlisha visiwa vya Reunion, Mauritius na Rodrigues kwa jina la visiwa vya Makareni. Visiwa hivi vilikuwa na umuhimu fulani kama vituo vya kupumzika katika safari kati ya Ulaya na Bara Hindi mabaharia wakitafuta maji ya kunywa, nafasi ya kutengeneza jahazi zao na kuongeza chakula. Lakini hapakuwa na makao ya kudumu kisiwani.

[edit] Utawala wa Kifaransa

Mwaka 1640 Wafaransa walivamia kisiwa na kukitangaza kuwa mali ya Ufaransa. Walikiita "Île Bourbon" kutokana na jina la familia ya wafalme wa Ufaransa. Mwaka 1665 walowezi wa kwanza Wafaransa walianza kujenga nyumba zao. Ufalme ulipoondelwa wakati wa mapinduzi ya Ufaransa kisiwa kimepewa jina jipya la Reunion tar. 17.03.1793. Wakati wa Vita za Napoleoni ndio Waingereza waliovamia kisiwa mwaka 1810 lakini kukirudisha kwa Wafaransa baada ya vita 1815.

Visiwa vya Makarena kati ya visiwa vya Kiafrika katika Bahari Hindi
Visiwa vya Makarena kati ya visiwa vya Kiafrika katika Bahari Hindi

[edit] Uchumi wa mashamba na watumwa

Walowezi wazungu walianzisha mashamba kwa ajili ya mahitaji ya jahazi zilizopita. Kuanzia mwaka 1718 mazao ya biashara yalilimwa , kwanza kahawa baadaye pia vanilla na hasa sukari. Kwa kusidi hiyo watumwa walipelekwa Reunion kutoka Afrika bara, Bara Hindi na Madagaska. Mwaka 1768 kisiwa kilikuwa na 26,284 wakazi huru hasa Wafaransa na watumwa 45,000. Ufaransa ulitia sahihi maazimio ya Mkutano wa Vienna 1815 pamoja na kumaliza biashara ya watumwa lakini biashara hii iliendela kwa siri na kupanuka hasa wafungwa kutoka Afrika. Idadi ya watumwa iliendela kuongezeka hadi kuondolewa hali ya utumwa tar. 20.12.1848. Baada ya mwisho wa utumwa walowezi walitafuta wafanyakazi huko Bara Hindi wakachukua wafanyakazi Wahindi wasiofika kama watu huru kwa miaka na haki kidogo. Baadaye hata wafanyakazi Wachina walichukuliwa.

[edit] Mkoa wa Ufaransa

Mwaka 1946 Reunion ilipewa cheo cha Mkoa wa Ufaransa, tangu 1997 imekuwa sehemu ya Umoja wa Ulaya. Mkoa wa Reunion ina wilaya (Kifaransa: arrondissements) nne.

[edit] Wakazi

Wakazi wanaonyesha historia hii katika mchanganyiko wao wa aina za watu na tamaduni kutoka pande mbalimbali wa dunia. Sehemu kubwa ya wakazi ni watoto wa watumwa au wafanyakazi wasio huru wa zamani wakinonyesha tabia za Wahindi, Waafrika na Wachina. Takriban robo ya wakazi ni wa asili ya Ulaya. Vikundi hivi havikai mbali kuna mchanganyiko wa kila aina. Wakazi wengi hufuata Ukristo wa kikatoliki, wengine Uislamu na Uhindu. Kuna pia Waprotestanti.


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad |Cote d'Ivoire | Djibouti | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia
Our "Network":

Project Gutenberg
https://gutenberg.classicistranieri.com

Encyclopaedia Britannica 1911
https://encyclopaediabritannica.classicistranieri.com

Librivox Audiobooks
https://librivox.classicistranieri.com

Linux Distributions
https://old.classicistranieri.com

Magnatune (MP3 Music)
https://magnatune.classicistranieri.com

Static Wikipedia (June 2008)
https://wikipedia.classicistranieri.com

Static Wikipedia (March 2008)
https://wikipedia2007.classicistranieri.com/mar2008/

Static Wikipedia (2007)
https://wikipedia2007.classicistranieri.com

Static Wikipedia (2006)
https://wikipedia2006.classicistranieri.com

Liber Liber
https://liberliber.classicistranieri.com

ZIM Files for Kiwix
https://zim.classicistranieri.com


Other Websites:

Bach - Goldberg Variations
https://www.goldbergvariations.org

Lazarillo de Tormes
https://www.lazarillodetormes.org

Madame Bovary
https://www.madamebovary.org

Il Fu Mattia Pascal
https://www.mattiapascal.it

The Voice in the Desert
https://www.thevoiceinthedesert.org

Confessione d'un amore fascista
https://www.amorefascista.it

Malinverno
https://www.malinverno.org

Debito formativo
https://www.debitoformativo.it

Adina Spire
https://www.adinaspire.com