Mkoa wa Mwanza
From Wikipedia
Mkoa wa Mwanza ni kati ya mikoa 26 za Tanzania. Umepakana na Kagera upande wa magharibi, Shinyanga upande wa kusini na Mara upande wa mashariki. Ziwa la Viktoria Nyanza liko kaskazini. Makao makuu ya mkoa yapo Mwanza mjini.
[edit] Wilaya
Mkoa wa Mwanza una wakazi 2,942,148 (sensa ya 2002) katika wilaya 8 ukiwa na eneo la 19,592km2. Wilaya ndizo Ukerewe,Magu, Sengerema, Geita, Misungwi, Kwimba, Nyamagana na Ilemela. Mji wa Mwanza umo ndani ya wilaya Nyamagana na Ilemela.
[edit] Wakazi
Makabila makubwa katika Mwanza ndio Wasukuma, Wakerewe, Wakara na Wazinza.
[edit] Viungo vya nje
- Mji wa Mwanza, habari za uchumi, utamaduni na mengi mengine
- Matokeo ya Sensa 2002 kwa Mwanza
- Serikali ya Tanzania
- Wasukuma
|
|
---|---|
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Iringa | Kagera | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Singida | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi | |