Mkoa wa Manyara
From Wikipedia
Mkoa wa Manyara ni kati ya mikoa 26 za Tanzania. Babati ndipo makao makuu ya mkoa. Umepakana na mikoa ya Arusha na Kilimanjaro upande wa kaskazini, Mkoa wa Tanga upande wa mashariki, Mkoa wa Dodoma upande wa Kusini na mikoa ya Singida na Shinyanga upande wa magharibi.
Mkoa wa Manyara imetengwa na Mkoa wa Arusha mwaka 2002 kwa azimio la rais wa jamhuri ukiwa na eneo la 46,359 km².
[edit] Wakazi
Jumla ya wakazi mkoani ilikuwa 1,040,461.Sensa ya 2002 Idadi imepatika katika wilaya zifuatazo (idadi ya wakazi katika mabano): Babati (303,013), Hanang (205,133), Mbulu (237,882), Simanjiro (141,676) na Kiteto (152,757)
Wenyeji wa mkoa huu ni pamoja na Wairaq, Wamasai, Wambulu na Wabarbaiq wakijihusisha na shughuli za kilimo na ufugaji kama njia ya kuingiza kipato chao cha kila siku.
Mkoa huu unayo majimbo ya uchaguzi yanayofikia (5) ambayo yanajumuisha majimbo ya, Babati, Kiteto, Hanang, Mbulu na Simanjiro.
[edit] Wilaya
Kuna wilaya zifuatazo: Mbulu, Babati, Hanang, Simanjiro and Kiteto.
[edit] Viungo vya nje
|
|
---|---|
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Iringa | Kagera | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Singida | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi | |