Mkoa wa Arusha
From Wikipedia
Mkoa wa Arusha ni moja kati ya mikoa ya Tanzania. Imepakana na Kenya upande wa kaskazini. Mikoa ya jirani ni kufuatana na mwendo wa saa: Kilimanjaro, Manyara, Shinyanga na Mara. Wilaya zake ni Monduli, Arumeru, Arusha, Ngorongoro na Karatu.
Eneo lake ni km za mraba 86,100 zikiwemo km² 2,460 za maji. Kati ya milima yake Oldoinyo Lengai ([2,878m) badi ni volkeno hai, Arusha ni Volkano ya kulala tangu mw. 1910. Mvua hunyesha kati ya millimita 1,800 mm kwa mwaka mlimani Arusha hadi 508 mm kwa mwaka katika maeneo makavu.
Mkoa wa Arusha ndio kitovu cha utalii Tanzania Bara. Barabara ya lami Daressalaam-Nairobi inavuka eneo lake. Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro wahudumia miji ya Arusha na Moshi. Kuna mbuga za taifa na hifadhi za wanyamapori Ngorongoro, Serengeti, Olduvai, Arusha, Tarangire na Ziwa Manyara. Hifadhi ya Mlima Kilimajaro iko karibu.
Arusha hulimwa kahawa, nafaka, pareto, katani, pamba, alizeti. Fosfati inachimbuliwa Minjingu Mkoani Arusha, na takribani tani 48,000 kwa mwaka hutumiwa katika uzalishaji wa mbolea.
Kati ya wakazi wa mkoa kiasili ndio Waarusha, Wameru, Wairaqw na Wamassai.
|
|
---|---|
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Iringa | Kagera | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Singida | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi | |