Mkoa wa Morogoro
From Wikipedia
Morogoro ni jina la mji, wilaya na mkoa wa Tanzania.
Mkoa wa Morogoro ni kati ya mikoa 26 ya Tanzania. Umepakana na mikoa ya Tanga, Pwani, Lindi, Songea, Iringa, Dodoma na Arusha. Ikiwa eneo lake ni 72 939 km² kuna wakazi 1,759,809 (mwaka 2002). Morogoro iko kati ya mikoa mikubwa zaidi ya Tanzania.
Mkoa una wilaya sita ndizo (idadi ya wakazi kwa mabano): Kilosa ( 489,513), Kilombero (322,779), Morogoro Vijijini (263,920), Morogoro Mjini (228,863), Mvomero (260,525), Ulanga (194,209). Wakazi walio wengi hukalia wilaya za kaskazini mkoani. Robo yao huishi katika miji ya mkoa.
Eneo la Mkoa wa Morogoro liko katikati ya mikoa ya pwani la Bahari Hindi na Nyanda za Juu. Kuna tambarare za chini kama vile Ifakara / Kilombero pia milima ya juu kama Uluguru penye mlima wa Kimhandu mwenye 2646 m juu ya UB.
Mito mikubwa ni Wami na Ruvu inayoanza kwenye milima ya Uluguru. Ruvu ndiyo mto wa kutoa maji ya Daressalaam.
Karibu nusu ya eneo la Mkoa wa Morogoro ni hifadhi za wanyama za Mikumi, Udzungwa na Selous.
Kabila kubwa ni Waluguru waliotoa jina kwa mji wa Morogoro pamoja na milima ya Uluguru. Makabila mengine makubwa zaidi ni Wangulu, Wakagulu, Wasagala na Wapogolo.
Barabara Kuu za lami za Daressalaam - Morogoro - Mbeya - Zambia/Malawi na Daressalaam - Morogoro - Dodoma hupita eneo la mkoa pamoja na reli ya kati Daresalaam - Morogoro - Dodoma - Kigoma / Mwanza. Reli ya TAZARA hupita wilaya ya Kilombero.
Kilimo kinategemea hali ya mvua. Kilombero kuna mashamba makubwa ya miwa. Mazao ya sokoni hulimwa milimani. Katibu nusu ya eneo la mashamba yote hulimwa mahindi.
|
|
---|---|
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Iringa | Kagera | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Singida | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi | |