Wikipedia:Site support
From Wikipedia
nchini tanzania shule nyingi sana zinaanzishwa zinaitwa kwa kiingereza 'english medium schools' kikubwa kinachofundishwa ni watoto wanaosoma hapo kujua kiingereza. sasa juhudi za taifa kukikuza kiswahili zitafanikiwa ikiwa watoto wetu au kizazi kijacho kitakuwa kimeegemea sana katika kujua kiingereza? matokeo yanaanza kuonekana sasa maneno mengi ya misamiati ya kiingereza yameingizwa katika kiswahili na lugha yetu imeonekana kama inategemea lugha nyingine katika matumizi. kingine ni kwanini watanzania wasomi wanaokijua kiswahili wasitafsiri vitabu vingi vya lugha za kigeni katika kiswahili ili visaidie katika kukuza lugha yetu?wakoloni walivyokuja walijitahidi sana kuzijua lugha zetu na wakafanikiwa mfano mzuri ni vitabu vinavyo tumika makanisani katika vijiji vya mikoa mbalimbali vingi wakoloni ndio walivyoviandika baada ya kijifunza lugha yetu kwa nini sisi tunaoijua vyema lugha yetu tusitafsiri vitabu kama vya Sayansi,teknolojia na vitabu vya elimu mbalimbali katika lugha yetu ili viweze kueleweka na wasomaji wengi na visaidie kukikuza kiswahili? ninaomba wadau wa maswala haya wajitahidi kutendea kazi
thabit mikidadi dar es salaam