Kuwait
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: (hakuna) | |||||
Wimbo wa taifa: watani alkuwait وطني الكويت سلمت للمجد (Taifa langu la Kuwait) |
|||||
Mji mkuu | Jiji la Kuwait |
||||
Mji mkubwa nchini | Salmiya | ||||
Lugha rasmi | Kiarabu | ||||
Serikali
Emir
Mrtihi wa cheo Waziri Mkuu |
Ufalme wa kikatiba Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah Nawaf Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah Nasser Al-Mohammed Al-Ahmed Al-Sabah |
||||
Uhuru kutoka Uingereza |
19 Juni 1961 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
17,818 km² (ya 157) -- |
||||
Idadi ya watu - 2006 kadirio - Msongamano wa watu |
3,100,0002 (--) 131/km² (ya 68) |
||||
Fedha | Kuwaiti Dinar (KWD ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC+3) (UTC+3) |
||||
Intaneti TLD | .kw | ||||
Kodi ya simu | +965 |
Kuwait (Kiar.: الكويت ) ni nchi ndogo ya Uarabuni kwenye pwani la Ghuba ya Uajemi. Imepakana na Irak na Saudia.
Nchi ni tajiri kutokana na uwingi wa mafuta ya petroli yaliyopo chini ya ardhi yake. Akiba zake nii kama 10% za akiba za dunia yote. Kabla ya kupatikana kwa mafuta mwaka 1938 nchi ilikuwa maskini lakini sasa ni kati ya nchi tajiri zaidi duniani.
Karibu nchi yote ni jangwa. Kabla ya kugunduliwa kwa mafuta palikuwa na kilimo kidogo sana halafu ufugaji na hasa uvuwi baharini.
Kati ya wakazi 2,600,000 nusu pekee ni wananchi au Wakuwait wenyewe. Wengine ni watu kutoka nchi jirani waliokuja kufanya kazi na kuishi hapo.
Historia ya Kuwait ilianza kama utemi mdogo chini ya familia ya Al-Sabah waliokuwa chini ya Sultani wa Uturuki aliyetawala nchi jirani ya Irak hadi vita kuu ya kwanza ya dunia. Tangu kuingia wa Waingereza katika nchi za ghuba watawala wa Kuwait walijiweka chini ya ulinzi wa Uingereza kwa sababu waliuona afadhali kuliko ukuu wa Uturuki. Baada ya kuporomoka wa dola la Uturuki Kuwait iliendelea chini ya Uingereza na kupata uhuru wake 1961.
Katika miaka iliyofuata Kuwait iliona madai ya Irak ya kuwa Kuwait ni mkoa wake tangu zamani uliotengwa na ukoloni. Mwaka 1990 dikteta wa Irak Saddam Hussein alivamia Kuwait tar. 2 Agosti 1990 na kuiteka. Katika vita ya pili ya ghuba Marekani pamoja na nchi nyingine ilishambulia jeshi la Irak katika Kuwait na kurudisha serikali ya Emir al Sabah.
Makala hiyo kuhusu "Kuwait" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Kuwait kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |