Afrika ya Mashariki
From Wikipedia
Afrika ya Mashariki ni sehemu ya bara la Afrika ambayo iko upande wa mashariki, ikipakana na Bahari ya Kihindi. Afrika ya Mashairiki ina nchi kadhaa ambazo ni Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi, Msumbiji, Somalia, Sudan, Jibuti, na Ethiopia, lakini nchi mashuhuri zaidi katika sehemu hii ni Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi kwa sababu ya kutumia lugha moja katika mawasiliano yao baina ya wananchi wa sehemu hii, yaani Kiswahili.
Aghalabu ya nchi za Afrika ya Mashariki zinazungumza lugha ya Kiswahili kama ndio lugha ya mawasiliano kati yao, kwani katika nchi hizi kuna makabila mengi sana na kila kabila lina lugha yake ambayo kawaida inatumika nyumbani baina ya watu wa kabila moja, lakini wakitaka kuwasiliana na makabila mengine, mara nyingi hutumia lugha ya Kiswahili, na hii ni kwa sababu lugha hii ndio iliyoenea zaidi na kufahamika zaidi katika eneo hili la dunia.
Wakazi wengi wa Afrika ya Mashariki ni wasemaji wa lugha za Kibantu; sehemu ya Kaskazini wasemaji wa lugha za Kihamiti ni wengi (Waoromo, Wasomalia). Katika Ethiopia kuna wasemaji wa lugha za Kisemiti.
Afrika ya Mashariki inatajwa na sayansi kuwa mahali ambako watu wa kwanza duniani walipopatikana.
Majina ya miji ya Afrika ya Mashariki imetajwa mara ya kwanza katika Periplus ya Bahari ya Eritrea katika karne ya kwanza b.K.
Mara nyingi hata nchi zifuatazo huhesabiwa kuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki:
- Malawi, Zambia na Zimbabwe – wakati mwingine zinehesabiwa kuwa sehemu ya Afrika ya Kusini au ya Afrika ya Mashariki - (zamani zilikuwa pamoja kama Rhodesia ya Kusini, Rhodesia ya Kaskazini na Unyasa katika Shirikisho la Afrika ya Kati)
- Komori, Morisi, Shelisheli, Mayotte na Réunion ni visiwa vidogo vya Bahari Hindi vinavyohesabiwa kuwa sehemu za Afrika ya Mashariki.
[edit] Ushirikiano wa nchi za Afrika ya Mashariki
Nchi za Afrika ya Mashariki, hasa Kenya, Uganda na Tanzania ni nchi ambazo ni karibu tangu zamani. Zimeshirikiana historia, zote zimekaliwa hasa na makabila yanayotumia lugha za Kibantu (Kenya na Uganda wana pia idadi muhimu ya wakazi wasiotumia lugha za Wabantu). Katika nchi zote tatu lugha ya Kiswahili imekuwa lugha muhimu ingawa kwa daraja mbalimbali. Wakati wa ukoloni zilitawaliwa na Uingereza iliyoacha taasisi na taratibu mbalimbali zilizosaidia kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wakati wa uhuru.
Tanzania, Kenya na Uganda zina ukubwa wa eneo la maili za mraba; Tanzania 360,000 ikifuatiwa na Kenya 224,960 na Uganda 93,980 upande wa mashariki nchi hizi zimepakana na bahari ya hindi na upande wa kaskazini mashariki zimepakana na Somalia upande wa kaskazini zimepakana na Ethiopia na Sudani upande wa magharibi ni Kongo na jamuhuri ya Rwanda na Burundi kusini ni Zambia; Malawi na Msumbiji.
Nchi hizi zimepitiwa na mstari wa ikweta, umepita Kenya na kusini mwa Uganda. Kenya na Tanzania zina ukanda wa pwani wenye bandari za Mombasa; Tanga; Bagamoyo; Dar-es-salaam; Zanzibar; Kilwa na Mtwara.
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad |Cote d'Ivoire | Djibouti | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia |