Lugha
From Wikipedia
Lugha (kar: لغة) ni utaratibu kwa ajili ya kuwasiliana kati ya binadamu au kati ya viumbe wo wote wenye akili.
Somo la lugha linaitwa maarifa ya lugha au isimu.
Contents |
[edit] Maana ya neno "lugha"
Mara chache neno lugha linatumika kwa taratibu za kuwasiliana za wanyama. Lakini taratibu hizo ni tofauti sana: Katika lugha za wanyama, sauti moja ina maana moja tu. Lakini katika lugha za binadamu, sauti nyingi zinaunganishwa kutengeneza maneno, na maneno mengi yanaunganishwa kutengeneza sentensi. Hivyo mnyama ambaye anaweza kutengeneza sauti ishirini tofauti anaweza "kusema" mambo ishirini tu. Kwa upande mwingine mtu ambaye anaweza kutengeneza sauti ishirini, anaweza kusema mambo zaidi ya millioni.
[edit] Aina za lugha
Kwa kawaida, lugha ni sehemu ya utamaduni wa umma fulani. Lugha ya aina hii inaitwa lugha asilia. Lakini pia kuna lugha za kuundwa.
[edit] Kukua na kufa kwa lugha
Tangu siku za kwanza za binadamu, lugha zimekuwa zikichipuka na kukuwa na kutangaa na kufa kama kiumbe chochote mwingine. Kwa hivyo, lugha zilizokuwepo leo ulimwenguni, huenda baada ya karne nyingi kupita zikatoweka na kuzuka nyenginezo.
Leo ulimwenguni mathalan, kuna lugha karibu 6,700, zikiwa 1,000 katika bara la kaskazini na kusini ya Marekani, 2,000 zikiwa kwenye bara la Afrika, 230 katika bara la Ulaya, 2,200 katika bara la Asia, na 1,300 katika bara la Oshania (Australia na nchi jirani nayo).
[edit] Kurasa zinazohusiana
- Lugha ya Kiarabu
- Lugha ya Kiesperanto
- Lugha ya Kiingereza
- Lugha ya Kiswahili
- Lugha asilia
- Lugha ya kuundwa