Ukoloni
From Wikipedia
Ukoloni ni mfumo wa taifa moja kuvuka mipaka yake na kutawala taifa jingine katika nyanja za kiuchumi, kiutamaduni na kijamii.
Nchi za Afrika yaliwekwa chini ya ukoloni wa nchi za Ulaya mara baada ya Mkutano wa Berlin ulioitishwa na chansella wa Ujerumani Bismarck mwaka 1884-1885.
Nchi zilizojenga ukoloni huu wa Afrika zilikuwa Uingereza, Ufaransa, Ureno, Ujerumani, Uhispania, Italia na Ubelgiji.
Ukoloni mamboleo ni aina ya nchi au kundi la nchi fulani kutawala nchi nyingine kinyemela kwa kuweka vikwazo na masharti yatakayowafanya watawaliwa waendelee kuwa na uchumi tegemezi ili wawatajirishe zaidi hao wanaowatawala kinyemela