Vita ya Marekani dhidi Hispania
From Wikipedia
Vita ya Marekani dhidi Hispania ilitokea mwaka 1898. Ilianza kwa shambulizi la Marekani tar. 25 Aprili dhidi ya Puerto Rico iliyokuwa koloni ya Hispania na kuishia tar. 12 Agosti 1898 jeshi la Hispania katika Manila (Ufilipino) lilipojisalimisha. Marekani ilitwaa koloni za Hispania za Puerto Rico, Kuba na Ufilipino.
Vita hii ilikuwa mwanzo wa Marekani kufuata siasa ya nje ya upanuzi hata katika maeneo ya mbali. Kabla ya vita hii Marekani ilishughulika kupanua eneo lake kwenye bara la Amerika ya Kaskazini dhidi ya wenyeji asilia na dhidi ya Mexiko.
Marekani ilitumia nafasi ya ghasia ya wenyeji wa Kuba dhidi ya utawala wa kikoloni ya Hispania. Baada ya mlipuko kwenye manowari ya Marekani USS Maine katika bandari ya Havana Marekani ilitangaza vita dhidi ya Hispania ingawa sababu ya mlipuko haikujulikana hadi leo ilikuwa nini. Hispania haikuweza kushindana na manowari na silaha za Marekani zilizokuwa zimeendelea kiteknolojia. Pia Marekani ilikuwa karibu na mahali pa vita na Hispania ilishindwa kuongeza wanajeshi au silaha.