Web - Amazon

We provide Linux to the World


We support WINRAR [What is this] - [Download .exe file(s) for Windows]

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
SITEMAP
Audiobooks by Valerio Di Stefano: Single Download - Complete Download [TAR] [WIM] [ZIP] [RAR] - Alphabetical Download  [TAR] [WIM] [ZIP] [RAR] - Download Instructions

Make a donation: IBAN: IT36M0708677020000000008016 - BIC/SWIFT:  ICRAITRRU60 - VALERIO DI STEFANO or
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Kiingereza - Wikipedia

Kiingereza

From Wikipedia

Kiingereza ni lugha ya Kigermanik cha Magharibi iliyokua nchini Uingereza. Leo, zaidi ya wasemaji wa lugha ya kwanza milioni mia nne wanazumgumza Kiingereza duniani. Watu wengi wanazumgumza Kiingereza kama lugha ya pili, kwa sababu ni lugha muhimu sana kwenye nyanja za sayansi na uchumi wa kimataifa.

Contents

[edit] Uenezaji wa Kiingereza

Kiingereza ni lugha rasmi ya pekee katika nchi za Uingereza, Marekani, Australia, New Zealand, Jamaica, na nchi nyingine. Kiingereza ni lugha rasmi pamoja na lugha nyingine katika nchi nyingi, kwa mfano Kanada (na Kifaransa), India (na Kihindi na lugha za majimbo), Ireland (na Kigaelik).

[edit] Kiingereza katika Afrika

Nchi nyingi za Afrika zinatumia Kiingereza kama lugha rasmi, lakini ni Waafrika wachache (isipokuwa Waafrika Kusini) ni wasema wa lugha wa kwanza. Nchi hizo ni Afrika Kusini, Ghana, Gambia, Lesotho, Liberia, Kamerun, Kenya, Namibia, Nigeria, Sierra Leone, Swaziland, Zambia na Zimbabwe. Kiingereza kinazumgumzwa pia nchini nyingine za Afrika ambapo sio lugha rasmi. Lugha nyingi za Afrika zimeazima maneno ya Kiingereza. Maneno haya yamerekebisha sauti ya lugha nyingine, kwa mfano: Kiingereza: train --> Kiswahili: treni.

[edit] Historia ya Kiingereza

[edit] Mwanzo wa lugha

Lugha ya Kiingereza imeanza huko Uingereza kutokana na kuingiliana kwa lugha mbalimbali hasa lugha za kale za Ujerumani, Denmark na Ufaransa.

Kusini ya kisiwa cha Uingereza ilikuwa sehemu ya Dola la Roma hadi mwanzo wa karne ya tano. Wenyeji walitumia lugha ya Kikelti pamoja na Kilatini ya Waroma, hasa mjini.

[edit] Uvamizi wa Waanglia-Saksoni: kuja kwa Kigermanik

Baada ya kuondoka kwa Waroma kisiwani makabila kutoka Ujerumani wa Kaskazini na Denmark walianza kuvamia kisiwa. Katika mwendo wa karne mbili waliteka sehemu kubwa ya Uingereza isipokuwa sehemu za magharibi kama vile Cornwall na Wales na sehemu za Kaskazini penye Waskoti. Wavamiaji walileta lugha zao za Kisaksoni na Kianglia (Ujerumani wa Kaskazini) zilizounganika kuwa lugha ya Kiingereza cha Kale. Inaonekena ya kwamba wenyeji walio wengi walianza kutumia lugha ya watawala wapya, wengine waliuawa au walihamia sehemu zisizo chini ya Waanglia-Saksoni.

Lugha hii iliathiriwa mara mbili. Kwanza ndio Wadenmark waliojaribu kujenga ufalme wao kisiwani. Waliteka sehemu za Uingereza ya Magharibi. Kiasi cha maneno kutoka lugha yao kimeingia Kiingereza cha kale kama Wales.

[edit] Uvamizi wa Wanormandy: kuja kwa Kifaransa, lugha mbili kando

Mwaka 1066 jeshi la Kinormandy kutoka Ufaransa wa Kaskazini walivamia na kuteka Uingereza. Wanormandy walikuwa wa asili ya Skandinavia lakini walikuwa wameshaanza kutumia lugha ya Kifaransa cha Kale. Wanajeshi hawa walikuwa mabwana wapya wa Uingereza wakitumia Kifaransa chao cha Normandy. Kwa karne kadhaa lugha mbili zilitumika kandokando: Kiingereza cha Kianglia-Saksoni cha watu wa kawaida na kile Kifaransa cha Kinormandy cha tabaka ya watawala. Kwa jumla watawala walianza kutumia lugha ya raia lakini lugha hii ilibadilika pia kwa kupokea maneno mengi kutoka kwa Kifaransa. Kuna makadirio ya kwamba zaidi ya theluthi moja ya maneno yote ya Kiingereza ni za asili ya Kifaransa.

[edit] Kuingiliana kwa lugha zote mbili: Kiingereza cha Kati

Kipindi hiki cha kuingiliana kati ya Kifaransa cha mabwana na lugha ya kawaida kimeleta Kiingereza cha Kati. Hadi leo asili ya maneno kutoka Kijerumani na Kifaransa ni wazi kabisa. Mfano mzuri ni maneno tofauti ya wanyama kadha na nyama yao: ng'ombe huitwa "cow" (sawa na Kijerumani wa Kaskazini "Kau") lakini nyama yake ni "beef" (kutokana neo la Kifaransa kwa ng'ombe "boeuf"); vilevile "sheep" kwa mnyama ya kondoo na "mutton" kwa nyama yake (Kijerumani ya Kaskazini: "Schaap" - Kifaransa: "mutton"), vilevile swine – pork (nguruwe) und calf – veal (ndama). Wakulima wafugaji walitumia lugha yao kwa mnyama - mabwana wasiogusa mnyama lakini kula nyama yake waliendelea kutumia neno la kifaransa kwa ajili ya mnyama yuleyule. Maneno yote mawili yaliingia katika Kiingereza cha Kisasa lakini kwa mambo mawili tofauti.

[edit] Kiingereza cha Kisasa

Kiingereza cha kisasa kimeanza na tafsiri ya Biblia ya William Tyndale baadaye na washairi wakuu kama William Shakespeare. Teknolojia ya uchapaji vitabu ilisambaza lugha hii nchini kote na kupunguza athira ya lahaja mbalimbali. Wakati ule Kiingereza kilipokea pia maneno mengi kutoka lugha za Kilatini na Kigiriki zilizokuwa lugha za taaluma na sayansi hadi karne ya 18 kote Ulaya.

Kiingereza cha kisasa cha leo kimeendelea kurahisisha lugha. Lakini urekebisho wa tahajia umeshindikana hadi leo hata kama kulikuwa na majaribio mbalimbali. Kutokana na historia yake Kiingereza kimebaki na tahajia isiyolingana na matamshi ya maneno. Mwandishi George Bernhard Shaw alionyesha tatizo hili kwa pendekezo la dhihaka: Neno la "fish" (samaki) liandikwe "ghoti": gh kama sauti ya "f" katika "cough", o kama sauti ya "i" katika "women", na ti kama sauti ya "sh" katika "nation".

[edit] Uenezaji wa Kiingereza duniani

Tangu karne ya 19 idadi kubwa ya wasemaji wa Kiingereza hawakuishi tena Unigerezea bali Marekani. Wakati wa karne ileile Kiingereza kilikuwa lugha ya utawala katika maeneo makubwa ya koloni za Dola la Uingereza. Baada ya koloni kuwa nchi huru mara nyingi Kiingereza kimeendela kuwa lugha rasmi za nchi hizi.

Kutokana na matukio haya yote Kiingereza kimekuwa leo lugha ya kwanza ya mawasiliano duniani hata kama si lugha yenye wasemaji wengi wa lugha ya kwanza.

[edit] Viungo vya nje

Our "Network":

Project Gutenberg
https://gutenberg.classicistranieri.com

Encyclopaedia Britannica 1911
https://encyclopaediabritannica.classicistranieri.com

Librivox Audiobooks
https://librivox.classicistranieri.com

Linux Distributions
https://old.classicistranieri.com

Magnatune (MP3 Music)
https://magnatune.classicistranieri.com

Static Wikipedia (June 2008)
https://wikipedia.classicistranieri.com

Static Wikipedia (March 2008)
https://wikipedia2007.classicistranieri.com/mar2008/

Static Wikipedia (2007)
https://wikipedia2007.classicistranieri.com

Static Wikipedia (2006)
https://wikipedia2006.classicistranieri.com

Liber Liber
https://liberliber.classicistranieri.com

ZIM Files for Kiwix
https://zim.classicistranieri.com


Other Websites:

Bach - Goldberg Variations
https://www.goldbergvariations.org

Lazarillo de Tormes
https://www.lazarillodetormes.org

Madame Bovary
https://www.madamebovary.org

Il Fu Mattia Pascal
https://www.mattiapascal.it

The Voice in the Desert
https://www.thevoiceinthedesert.org

Confessione d'un amore fascista
https://www.amorefascista.it

Malinverno
https://www.malinverno.org

Debito formativo
https://www.debitoformativo.it

Adina Spire
https://www.adinaspire.com