Usanifu
From Wikipedia
Usanifu majengo ni sanaa na sayansi ya kubuni muundo na sura ya majengo. Sanaa na sayansi hii inajumuisha pia mambo kama mipango miji, usanifu wa eneo la kujenga, na hata ubunifu wa samani zitakazotumika ndani ya jengo.
Watu wanaojihusisha na haya huitwa "wasanifu". Wanahitaji elimu ya ujenzi, mahesabu, sanaa, teknolojia, elimu jamii na historia.
Mbini za usanifu hutegemea teknolojia inayopatikana, hali ya hewa, hali ya jamii, utaratibu wa siasa yake, hali ya uchumi na mengi mengine.
Nchi na tamaduni mbalimbali ziliunda aina tofauti za usanifu.