Teknolojia
From Wikipedia
Teknolojia ni elimu inayohusu uhandisi, ufundi, vifaa na mbinu za uzalishaji wa vifaa na huduma katika jamii.
Asili ya neno ni Kigiriki "τέχνη" (tamka: tékhne): „uwezo, usanii, ufundi".
Teknolojia inaweza kumaanisha:
- vifaa na mashine zinazotumika katika matengenezo au uzalishaji wa vitu
- elimu ya matumizi yake pamoja na mbinu na maarifa jinsi ya kutumia sayansi