Ujenzi
From Wikipedia
Ujenzi ni teknolojia ya kujenga nyumba, viwanda, barabara, daraja au hata miji. Ujenzi ni kazi inayohusisha watu wengi na ngazi mbalimbali ya kupanga na kutekeleza.
Majengo madogo yajengwa na watu wenyewe kufuatana na maarifa yao bila mpangilio mkubwa. Wajenzi hutumia maarifa ya watu waliowatangulia.
Majengo makubwa zaidi huhitaji mpangilio mwangalifu. Mwenye jengo atatafuta kwanza ushauri wa wataalamu.
Msanifu atachora ramani. Wataalamu wengine hukadiria mahitaji ya vifaa na gharama za jengo. Vibali vinahitajika.
Wajenzi watakaa na kupanga mahitaji ya muda, pesa, wafanya kazi na mashine. Wahandisi na mafundi wa fani mbalimbali hushirikiana.
Utekelezaji unasimamiwa na msanifu pamoja na wataalamu wengine. Ni muhimu kuhakikisha ubora wa vifaa vinavyotumika wakati wa kujenga kwa kila hatua. Vipimo vinapaswa kufuatwa kwa umakini. Kama msingi una makosa jengo lote linaweza kukaa bila kumalizika wakati gharama kubwa zimeshapotea.
Jengo zuri litakaa muda mrefu. Lakini hakuna majengo ya kisasa itakayodumu kama piramidi za Misri!