Web - Amazon

We provide Linux to the World


We support WINRAR [What is this] - [Download .exe file(s) for Windows]

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
SITEMAP
Audiobooks by Valerio Di Stefano: Single Download - Complete Download [TAR] [WIM] [ZIP] [RAR] - Alphabetical Download  [TAR] [WIM] [ZIP] [RAR] - Download Instructions

Make a donation: IBAN: IT36M0708677020000000008016 - BIC/SWIFT:  ICRAITRRU60 - VALERIO DI STEFANO or
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Nyotamkia - Wikipedia

Nyotamkia

From Wikipedia

Nyotamkia inayoitwa "West"
Nyotamkia inayoitwa "West"
Njia ya nyotamkia ikizunguka jua. Mkia huelekea mbali na jua kila wakati
Njia ya nyotamkia ikizunguka jua. Mkia huelekea mbali na jua kila wakati

Nyotamkia (kometi) ni gimba dogo la angani linalozunguka jua kwa njia ya duaradufu yenye sehemu kubwa mbali na jua na sehemu ndogo karibu na jua. Pale inapokaribia jua inaotesha "mkia" unaoipa jina lake la "nyota yenye mkia". Mkia huu ni hasa mvuke inayong'aa kutokana na nuru inayoakisiwa.

Mwili wa nyotamkia ni mchanganyiko wa mawe, vumbi na barafu. Muda mwingi nyotamkia iko mbali na jua hata haionekani kwa darubuni. Ikifuata njia ya mzunguko na kukaribia jua kiasi cha kutosha inaanza kuonekana kama nyota ikiakisi nuru ya jua. Ikikaribia jua zaidi sehemu ya barafu yake inaanza kuyeyuka kuwa mvuke unaoachana na nyotamkia mwenyewe na kuonekana kama "mkia". Mkia huu unaelekea kila wakati upande usio wa jua kwa sababu upepo wa jua unapuliza mvuke upande ule.

Kati ya nyotamkia ni kadhaa tu zinazokaribia kiasi cha kutosha hadi zinaonekana kuwa na mkia kwa macho tu kwa muda wa wiki hadi miezi kadhaa. Zamani ziliaminiwa kuwa ishara kutoka mbinguni au kutoka Mungu zikisababisha wasiwasi na hofu.

[edit] Historia

Nyotamkia zimetambuliwa kuwa magimba yanayorudi baada ya muda fulani. Mara ya kwanza nyotamkia ya "Halley" ilitambuliwa na Mwingereza Edmond Halley mwaka 1705 ya kuwa inarudi. Halley alitambua ya kwamba nyotamkia aliyoiona mwaka 1705 ilikuwa ileile iliyowahi kuonekana mwaka 1682. Alitabiri ya kwamba nyotamkia hii itaonekana tena mwaka 1759 ikawa hivyo. Nyotamkia hii imepewa jina la "Halley" imeendelea kurudi kila baada ya miaka 76. Wanahistoria waliweza kuthebitisha ya kwamba taarifa mbalimbali katika historia kuhusu nyotamkia tangu mwaka 240 BK ziliihusu "Halley". Ilipoonekana mwaka 1985/86 nuru yake ilikuwa imepungua kulingana na ziara za awali kutokana na kupungua kwa mada yake iliyopotea katika "mkia".

Leo kuna nyotamkia takriban 170 zilizothebitishwa ya kuwa zimerudi. Kuna pia nyotamkia chache zilizoonekana kwa darubini jinsi zilivyopasuka na kwisha wakati wa kupita karibu na jua.

Kutokana na habari hizo zote wataalamu hufukiri ya kwamba kuna nyotamkia nyingi katika mfumo wa jua letu lakini idadi inaendelea kupungua polepole zikikwisha kutokana na kupungua kwa mada au kutokana na kukaribia mno kwenye jua au hata kutokana na kugongana na magimba mengine. Haiwezekani kujua idadi kwa sababu muda wa kuzunguka jua ambao ni sawa na muda wa kuonekana tena unaweza kuwa miaka mamia hivyo nyingine haikuonekana bado tangu mwanzo wa falaki ya kisayansi.

Our "Network":

Project Gutenberg
https://gutenberg.classicistranieri.com

Encyclopaedia Britannica 1911
https://encyclopaediabritannica.classicistranieri.com

Librivox Audiobooks
https://librivox.classicistranieri.com

Linux Distributions
https://old.classicistranieri.com

Magnatune (MP3 Music)
https://magnatune.classicistranieri.com

Static Wikipedia (June 2008)
https://wikipedia.classicistranieri.com

Static Wikipedia (March 2008)
https://wikipedia2007.classicistranieri.com/mar2008/

Static Wikipedia (2007)
https://wikipedia2007.classicistranieri.com

Static Wikipedia (2006)
https://wikipedia2006.classicistranieri.com

Liber Liber
https://liberliber.classicistranieri.com

ZIM Files for Kiwix
https://zim.classicistranieri.com


Other Websites:

Bach - Goldberg Variations
https://www.goldbergvariations.org

Lazarillo de Tormes
https://www.lazarillodetormes.org

Madame Bovary
https://www.madamebovary.org

Il Fu Mattia Pascal
https://www.mattiapascal.it

The Voice in the Desert
https://www.thevoiceinthedesert.org

Confessione d'un amore fascista
https://www.amorefascista.it

Malinverno
https://www.malinverno.org

Debito formativo
https://www.debitoformativo.it

Adina Spire
https://www.adinaspire.com