Fridtjof Nansen
From Wikipedia
Fridtjof Nansen (10 Oktoba, 1861 – 13 Mei, 1930) alikuwa mpelelezi wa maeneo ya ncha ya Kaskazini, mwanazuolojia na mwanasiasa kutoka nchi ya Norwei. Katika safari yake ya miaka 1888-89 alikuwa mpelelezi wa kwanza kuvuka kisiwa cha Greenland kutoka Mashariki kwenda Magharibi. Miaka ya 1893-96 alisafiri na meli yake iliyoitwa Fram ndani ya barafu ya Bahari ya Ncha ya Kaskazini. Miaka ya 1906-08 alikuwa balozi ya Norwei kule London, Uingereza. Mwaka wa 1922 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani.