Charles Nicolle
From Wikipedia
Charles Jules Henry Nicolle (21 Septemba, 1866 – 28 Februari, 1936) alikuwa daktari kutoka nchi ya Ufaransa. Hasa alichunguza virusi visababishavyo magonjwa mbalimbali. Alikuwa wa kwanza kueleza jinsi ya kuenea kwa homa ya madoa madoa. Mwaka wa 1928 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.