Kanada
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: Kilatini: A Mari Usque Ad Mare ("Bahari hadi bahari") |
|||||
Wimbo wa taifa: "O Canada" Wimbo wa kifalme: "God Save the Queen" |
|||||
Mji mkuu | Ottawa |
||||
Mji mkubwa nchini | Toronto | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza, Kifaransa | ||||
Serikali
Mfalme (malkia) Gavana Mkuu Waziri mkuu |
Ufalme, shirikisho, demokrasia Malkia Elizabeth II Michaëlle Jean Stephen Harper |
||||
Uhuru Sheria ya 1867 Mkataba wa Westminster Sheria kuhusu Kanada |
1 Julai 1867 11 Desemba 1931 17 Aprili 1982 |
||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
9,984,670 km² (ya 2) 8.92 (891,163 km²) |
||||
Idadi ya watu - 2006 kadirio - 2001 sensa - Msongamano wa watu |
32,623,490 (ya 36) 30,007,094 3.2/km² (ya 219) |
||||
Fedha | Dollar ya Kanada ($) ( ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-3.5 to -8) (UTC-2.5 to -7) |
||||
Intaneti TLD | .ca | ||||
Kodi ya simu | +1 |
Kanada ni nchi kubwa ya Amerika ya Kaskazini. Mji mkuu ni Ottawa. Ni nchi kubwa duniani baada ya Urusi lakini idadi wa wakazi ni milioni 32 tu. Kwenye nchi kavu imepakana na Marekani bara na jimbo la Alaska. Mbele ya pwani zake kuna kisiwa kikubwa cha Greenland ambayo ni chini ya Denmark halafu visiwa vidogo vya St. Pierre na Miquelon (Ufaransa).
[edit] Jiografia
Kanada ni nchi kubwa ya pili duniani lakini maeneo mengi ni baridi mno hawana watu. Pwani la Kanada ni ndefu kushinda nchi zote za dunia ikipakana na Atlantiki, Pasifiki na Bahari ya Aktika.
Jumla ya wakazi milioni 32 huishi katika majimbo 10 na maeneo matatu ya kitaifa.
Katika eno la 9,984,670 km² ni 9,093,507 km² nchi kavu na 891,163 km² maji. Umbali kutoka Rasi Columbia kwenye kisiwa cha Ellesmere katika kaskazini hadi kisiwa cha kisiwa cha Middle Island katika ziwa la Erie jimboni Ontaria ni 4,634 km.
Umbali kutoka Rasi Spear katika Newfoundland upande wa mashariki hadi mpaka na Alaska upande wa magharibi ni 5,514 km.
[edit] Miji
Zaidi ya nusu ya wakazi hushi katika miji mikubwa zaidi. Mji mkubwa ni Toronto yenye wakazi milioni 5.6 ambayo ni bandari kwenye Ziwa Ontario na kitovu cha viwanda. Montreal ni mji wa biashara mwenye milioni 3.27.
Miji mingine mikubwa ni (idadi ya wakazi katika mabano):
- Vancouver (2.130.000)
- Calgary (968.475)
- Ottawa (874.433)
- Edmonton (822.319)
- Québec (745.623)
- Hamilton (653.637)
- Winnipeg (632.069 Ew.).
[edit] Historia
Maneo ya Kanada yalikaliwa tangu miaka 50,000 hadi 15,000 iliyopita na wahamiaji kutoka Asia ya Kaskazini.
Wazungu wa kwanza waliofika walikuwa Wanorwei kutoka Greenland mnamo mwaka 1000 BK. Lakini hawakukaa muda mrefu sana. Katika karne zilizofuata kuna uwezekano ya kwamba wavuwi kutoka Ulaya ya Kaskazini walifika pwani za Kanada mara kwa mara na kujenga makazi ya muda wakikausha samaki kwa ajili ya sfari za kurudi lakini hakuna uhakika.
26 Aprili 1497 alifika Mwitalia Giovanni Caboto (kwa Kiingereza huitwa "John Cabot") kwenye visiwa vya Newfoundland akiwa katika utumishi wa malkia wa Uingereza akavitangaza kuwa eneo la Kiingereza.
Mnamo 1534/1535 Wafaransa walifika katika eneo la Mto Saint Lorensi na kujenaga makao yao.
Wapelelezi na walowezi kutoka Ulaya walileta nao magonjwa ambayo hayakujulikana kwa wenyeji asilia na kusababisha vifo vingi kati yao. Kupunguzwa kwa wakazi asilia kulisaidia upanuzi wa walowezi Wazungu kota Amerika.
Koloni za Waingereza na Wafaransa zilikua polepole. Katika Vita ya Miaka Saba Ufaransa ilipotea maeneo yake yote yaliyotwaliwa na Uingereza. Visiwa vya St. Pierre na Miquelon pekee vilibaki upande wa Ufaransa. Uingereza iliamua kukubali utamaduni wa pekee wa wakazi Wafaransa katika jimbo la Quebec. Hadi leo wanaendelea kutumia Kifaransa na kufuata hasa Ukatoliki tofauti na Wakanada wenye asili ya Kiingereza walio zaidi Waprotestanti.
Wakati wa vita ya kupigania uhuru wa Marekani wakazi wa Kanada walibaki upande wa Uingereza. Hivyo Kanada iliendelea chini ya Uingereza ikaitwa "Amerika ya Kaskazini ya Kiingereza".
1841 sehemu mbaimbali ziliunganishwa kama koloni moja ya Kanada. 1867 Bunge la Uingereza lilikubali sheria iliyounda Shirikisho la Kanada lenya majimbo manne ya Ontario, Quebec, Nova Scotia na New Brunswick. Sasa Kanada ilikuwa nchi ya kujitawala chini ya Mfalme wa Uingereza.
Kujengwa kwa reli kati ya Atlantiki na Pasiki na kufika kwa wahamiaji kutoka Ulaya kuliimarisha nchi mpya. Majimbo mapya yaliundwa hadi kufika majimbo 10 na maeneo matatu chini ya shirikisho jinsi ilivyo sasa.
Kanada ilishikamana na Uingereza katika vita kuu za dunia zote mbili. Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia nchi ilionekana kama nchi ya pekee iliyotoa sahihi yake pekee na Uingereza chini ya mkataba wa Versailles. 1927 ilimpeleke balozi wa kwanza Marekani. Uhuru kamili ilipatikana 1982.
Makala hiyo kuhusu "Kanada" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Kanada kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |