Nairobi
From Wikipedia
Nairobi ni mji mkuu wa Kenya na vilevile mojawapo ya mikoa ya Kenya. Ni kati ya miji mikubwa ya Afrika ukiwa na wakazi wapatao milioni 3 katika eneo la 150 km². Jina Nairobi limetokana na neno la Kimaasai, Enkarenairobi, linalomaanisha "mahali penye maji baridi."
Lugha zote za Kenya huzungumzwa Nairobi lakini hasa ni Kiingereza na Kiswahili, pamoja na Sheng.
Eneo lake, hali ya hewa
Nairobi imeanzishwa mahali ambako nchi tambarare ya Athi inakutana na mtelemko wa nyanda za juu zinazoongozana na Bonde la Ufa. Kitovu cha Nairobi iko zipatao 1624 m juu ya UB. Mahali pake ni kama 150 km kusini mwa ekweta. Hali ya hewa haina joto kali. Halijoto ya wastani ni 20,5° mwezi wa Machi, na 16,8° mwezi wa Julai. Mvua nyingi hunyesha mwezi wa Machi (199 mm), kiangazi ina 14mm tu wakati wa Julai.
Historia ya Nairobi
Nairobi imeanzishwa mw. 1899 na Waingereza kama kambi ya kujenga Reli ya Uganda. Mahali ilikuwa karibu katikati ya Mombasa na Kampala, palikuwa na maji ikaonekana ilifaa kwa kituo njiani. Mwanzo wa Nairobi ilikuwa kambi kubwa ya hema na ghala za vifaa vya kujenga reli. Mwanzoni viongozi wengine walitaka kuacha eneo hili kwa sababu ya matope mengi. Lakini makao iliendelea kukua nyumba za mawe zikajengwa. Mw. 1905 Waingereza walihamisha ofisi kuu ya serikali yao ya kikoloni kutoka Mombasa kwenda Nairobi ikawa makao makuu ya Afrika ya Mashariki ya Kiingereza (British East Africa Protectorate, baadaye Kenya Colony).
1963 ikawa mji mkuu wa nchi huru ya Kenya.
Ikaendelea kukua haraka.
NAIROBI YA LEO
Nairobi imeibuka kua mojawapo ya miji mikubwa katika bara la afrika. Mashirika mengi makubwa duniani yamefungua ofisi zao zinazoshuhudia eneo la afrika mashariki na afrika ya kati. moja wapo ya hayo ni ofisi za mojawapo ya tawi la umoja wa mataifa (united nations), UNEP. kunazo pia ofisi za mabalozi wa nchi mbali mbali duniani. Nairobi, kama miji mingi mikubwa, ina matatizo mengi yanayotokea kwa sababu ya ukubwa wake. Watamaduni walioupanga mji wa nairobi hawakutegemea kua ungenenepa hivyo. Wataalamu wengi wame toa maoonyo mengi kuhusu ukubwa wa mji na uwezo wake wa kuwashuhudia waakaazi wote ambao wanazidi kuongezeka kila mwaka. Nairobi imewavutia waakaazi wengi wote wakiwa na hamu ya kujitafutia riziki yao. ijapokuwa kunao wanaofanikiwa, wengi wao hujipata wameangulia patupu wakawachwa bila pesa au hali ya kujitegemea. jambo hili limeleta ongezeko kwa wakaaji wa maeneo yasiotengwa kwa wananchi au 'slums' kwa kimombo. eneo kubwa kabisa jijini nairobi ki eneo la kibera. eneo hili lina ukubwa wa kilomita 2 kwa 2 na wakaazi takribani milioni moja. eneo hili halina mipango yeyote ya kuruhusu binadamu kuishi lakini umaskini umewavutia wengi kuishi kule.
kunayo pia matatizo ya ujambazi wa kibinafsi, ujambazi wa nyumba na utekaji nyara wa magari. Matatizo haya yamesababisha watu wengi kutoupendelea mji wa nairobi.
|
|