Honduras
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: Libre, Soberana e Independiente |
|||||
Wimbo wa taifa: „Tu bandera es un lampo de cielo“ (wewe bendera u nuru ya angani) |
|||||
Mji mkuu | Tegucigalpa |
||||
Mji mkubwa nchini | Tegucigalpa | ||||
Lugha rasmi | Kihispania | ||||
Serikali
Rais
|
Jamhuri, demokrasia Manuel Zelaya |
||||
Uhuru Imetangazwa imetambuliwa |
15 Septemba 1821 1823 |
||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
112,492 km² (ya 102) (kidogo sana) |
||||
Idadi ya watu - Julai 2006 kadirio - 2000 sensa - Msongamano wa watu |
7,326,496 2 (ya 96) 6,975,204 64/km² (ya 128) |
||||
Fedha | Lempira (HNL ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-6) (UTC) |
||||
Intaneti TLD | .hn | ||||
Kodi ya simu | +504 |
Honduras ni nchi ya Amerika ya Kati. Imepakana na Guatemala, El Salvador na Nikaragua. Upande wa kusini ina pwani fupi la Pasifiki na upande wa kaskazini pwani ndefu la Bahari ya Karibi.
Contents |
[edit] Jiografia
Honduras ni nchi ya milima mingi inayopanda hadi kimo cha Cerro Las Minas chenye 2849 m juu ya UB.
Hali ya hewa ni kitropiki lakini joto inapoa milimani.
[edit] Miji
Mji mkuu na mji mkubwa mwenye wakazi milioni 1.09 ni [Tegucigalpa]]. Miji minhine mikubwa kiasi ni San Pedro Sula (wakazi 491,000) katika kaskazini-magharibi, halafu miji ya bandari ya La Ceiba (wakazi 111,000) na Puerto Cortés (wakazi 36,000).
[edit] Mito na maziwa
Mito mingi ya Honduras huelekea Atlantiki. Río Patuca na Río Ulúa ni mito mirefu ya nchi. Ziwa kubwa la Lago de Yojoa lenye eneo la 285 km² ni muhimu kwa ajili ya ajili ya maji ya miji.
[edit] Wakazi
Idadi ya wakazi ni takriban milioni 14 hivyo ni nchi yenye wakazi wengi katika Amerika ya Kati. Wakazi walio wengi wengi kabisa ni machotara hasa wenye asili ya mchanganyiko wa wazalendo na Wazungu. Hao ndio aslilima 90 ya wakazi. Katika misitu ya milimani kuna bado vikundi vya wenyeji asilia (Wahindi wekundu). Wengine ni wa asili ya Afrika au ya Ulaya wasiochanganyika sana na wengine. Kwneye pwani la kaskazini kuna makazi ya Wagarifuna ambao ni utamaduni wa mchanganyiko wa Wahindi wekundu na Waafrika.
[edit] Historia
Honduras ilikuwa sehemu ya maeneo ya Wamaya. Lakini miji yao ilikwaisha tayari kabla ya kufika kwa Wahispania. Kristoforo Kolombo alifika mwaka 1502 karibu na Trujillo katika kaskazini na kuita nchi "Honduras" (=Kihisp. vilindi) kwa sababu ya maji marefu mwambanoni.
1524/1525 Wahispania walianza kuvamia nchi na kuunda mji wa Comayagua mwaka 1540. Mji mkuu wa leo ulianzishwa mwaka 1579 kama kituo cha kuchimba madini kama dhahabu na fedha.
1821 Honduras ilijiunga na ghasia ya maeneo mengine ya Amerika ya Kati dhidi ya utawala wa Hispania. Mwanzoni nchi hizi ndogo zilijiunga na Meksiko lakini baada ya miaka miwili zilianzisha "Shirikisho la Amerika ya Kati" iliyokwisha mwaka 1839. Tangu mwaka ule Honduras imekuwa nchi ya kujitegemea kabisa.