Frederic Passy
From Wikipedia
Frederic Passy (20 Mei, 1822 – 12 Juni, 1912) alikuwa mtaalamu wa uchumi kutoka nchi ya Ufaransa. Anajulikana hasa kwa maandishi yake yaliyojaribu kuzuia vita. Mwaka wa 1901, pamoja na Henri Dunant, alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel kwa Amani.