Limpopo (mto)
From Wikipedia
Mto wa Limpopo | |
---|---|
|
|
Chanzo | Milima ya Witwatersrand katika Gauteng nchini Afrika Kusini |
Mdomo | Bahari ya Hindi |
Nchi | Afrika Kusini, Botswana, Zimbabwe na Msumbiji. |
Urefu | 1,600 km au 1,800km |
Kimo cha chanzo | takriban 1,700 m |
Mkondo | 800 m³/s |
Eneo la beseni | 414,524 km² |
Limpopo ina chanzo chake katika mto wa Krokodil (Kiafrikaans: mamba) katika milima ya Witwatersrand kati ya Pretoria na Johannesburg nchini Afrika Kusini. Inapita mwendo wa pinde kubwa ikielekea kwanza kaskazini-magharibi halafu mashariki hadi Bahari Hindi.
Baada ya kupokea mto wa Marico huitwa kwa jina Limpopo. Baadaye inafuata mpaka kati ya Afrika Kusini na Botswana halafu mpaka wa Afrika Kusini na Zimbabwe.
Tawimto mkubwa ni mto wa Olifant (Kiafrikaans: tembo) unaojiunga na Limpopo katika Msumbiji 200km kabla ya mdomo wake. Moto unafikia Bahari Hindi kwa mji wa Xai-xai.