Pretoria
From Wikipedia
Pretoria ni moja kati ya miji mikuu mitatu ya Afrika Kusini na makao makuu ya serikali. Miji mikuu mingine ni Cape Town kama makao ya Bunge na Bloemfontein kama makao ya Mahakama Kuu.
Pretoria iko katika kaskazini ya jimbo la Gauteng katika bonde la milima ya Magalies kwenye kimo cha 1,370 m. Umbali na Johannesburg ni 56 km. Ni sehemu ya Jiji la Tshwane.
Jina la Pretoria ni la kumkumbusha jenerali ya Makaburu Andries Pretorius aliyeshinda Wazulu kwenye mapigano ya Mto wa Damu (Blood River) 1838. Kuna majadiliano kama jina la Pretoria libadilishwe pia kuwa "Tshwane".
Pamoja ofisi za serikali kuna vyuo vikuu hasa Chuo Kikuu cha Pretoria. Chuo Kikuu cha Afrika Kusini ni chuo kikubwa cha masomo kwa njia ya barua.
Makala hiyo kuhusu "Pretoria" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Pretoria kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |