UNESCO
From Wikipedia
UNESCO ni kifupi cha United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization au Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa ni kitengo cha Umoja_wa_Mataifa. Inashughulika habari za elimu, sayansi na utamaduni duniani.
Kisheria UNESCO ni shirika la kujitegemea lenye madola wanachama 191.
Kati ya shughuli muhimu za UNESCO ni Orodha la Urithi wa Dunia linalojumlisha mahali penye umuhimu wa pekee kihistoria, kisayansi au kiutamaduni. Nchi zote zina mahali angalau moja orodhani, nyingine zina pengi.