Oresund
From Wikipedia
Oresund (Kidenmark: Øresund, Kiswidi: Öresund) ni mlango wa bahari unaotenganisha kisiwa cha Zealand (Sjælland) katika Denmark na jimbo la Skania (Skåne) katika Uswidi.
Oresund ni moja kati ya milango mitatu ya bahari inayopita katika visiwa vya Denmark na kuunganisha Bahari ya Kaskazini na Bahari ya Baltiki kwa njia ya Kattegat na Skagerak. Ni kati ya njia za bahari duniani zenye meli nyingi sana.
Tangu mwaka 2000 kuna daraja la kuvukia Oresund kutoka Denmark kwenda Uswidi. Lilifunguliwa rasmi tarehe Julai 1 mwaka 2000 na mfalme Carl XVI Gustav wa Uswidi na malkia Margrethe II wa Denmark.
[edit] Viungi vya nje.
- Oresundskonsortiet - Official web site of the bridge builders
- Oresunddirekt - Official public information site for the inhabitants of the Oresundregion