Skagerak
From Wikipedia
Skagerak ni mlango wa bahari kati ya Norway na Denmark karibu na mji wa Skagen. Skagerak inahesabiwa kuwa sehemu ya Bahari ya Kaskazini. Upande wa Mashariki inaanza Kattegat.
Karibu na pwani la Norway kuna mfereji wenye kina kubwa hadi 770 m chini ya UB. Mafuta na gesi zinapatikana kwa njia ya pampu kutoka eneo chini ya bahari.