Kattegat
From Wikipedia
Kattegat ni mlango wa bahari katika Ulaya ya kaskazini kati ya rasi ya Jutland ya Denmark na pwani la Uswidi (Sweden).
Kattegat ni sehemu ya njia ya kuunganisha Bahari ya Kaskazini na Bahari ya Baltiki. Kaskazini yake iko Skagerak na kusini milango ya Oresund na Belt Mkubwa.
Bahari haina kina kubwa lakini kuna usafiri mwingi wa meli za kila aina. Machafuko wa maji kutokana na mbolea wa kilimo yamesababisha kupungua sana kwa samaki katika sehemu hii.