Masedonia
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: {{{national_motto}}} | |||||
Wimbo wa taifa: Денес над Македонија Leo juu ya Masedonia |
|||||
Mji mkuu | Skopje (tamka: "skopye" |
||||
Mji mkubwa nchini | Skopje | ||||
Lugha rasmi | Kimasedonia, Aialbania1 | ||||
Serikali
Rais
Waziri Mkuu |
Parliamentary Jamhuri Branko Crvenkovski Nikola Gruevski |
||||
Independence Ilitangazwa |
8 Septemba 1991 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
25,333 km² (ya 148) 1.9 |
||||
Idadi ya watu - 2005 kadirio - Msongamano wa watu |
2,034,000 (ya 143) 79/km² (ya 110) |
||||
Fedha | Denar ya Masedonia (MKD ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) |
||||
Intaneti TLD | .mk | ||||
Kodi ya simu | +389 |
||||
1Kimasedonia ni lugha rasmi ya kwanza. Kialbania ni lugha rasmi ya pili pamoja na Kimasedonia; kila lugha inayotumiwa na 20% ya wakazi hutumiwa kama lugha rasmi ya nyongeza kimahal kama vile Kituruki, Kiserbia, Kiromany na Kiaromania. |
Masedonia ni nchi kwenye rasi ya Balkani katika Ulaya ya kusini mashariki. Imepakana na Serbia, Albania, Ugiriki na Bulgaria. Rasmi nchi inajiita Jamhuri ya Masedonia (Република Македонија / Republika Makedonija, Republika e Maqedonisë). Jina rasmi la kimataifa ni "Masedonia iliyokuwa jamhuri ya Yugoslavia" (tazama chini).
Mji mkuu ni Skopje yenye wakazi 600,000. Miji midogo zaidi ni pamoja na Bitola, Prilep, Tetovo, Kumanovo, Ohrid, Veles, Štip, Gostivar na Strumica.
Masedonia ni nchi mwanachama ya Umoja wa Mataifa na inasubiri kupokelewa katika Umoja wa Ulaya.
[edit] Historia
Masedonia ni eneo linalokaliwa hasa na Waslavoni wanaozungumzwa lugha iliyo karibu na Kibulgaria na Kiserbia. Eneo hili lilitawaliwa kwa muda mrefu na Dola la Uturuki. Si rahisi kujua watu wa sehemu hizi walianza lini kujisikia kama watu tofauti na wa pekee na majirani yao hasa Wabulgaria. Inaonekana hii ilitokea hasa wakati wa karne ya 20.
Masedonia ya leo ilikuwa jimbo la kujitawala la Yugoslavia. Baada ya mwisho wa shirikisho la Yugoslavia Masedonia naye ilitafuta uhuru wake. Mwanzoni palikuwa na matatizo ya kutumia jina kwa sababu ya upinzani wa Bulgaria na Ugiriki zinazodai kuwa "Masedonia" ni sehemu ya urithi wao wa kitaifa. Kwa muda nchi ilijulikana rasmi kama "Masedonia iliyokuwa jamhuri la Yugoslavia" lakini yenyewe inajiita "Jamhuri ya Masedonia".
[edit] Wakazi na utamaduni
Wamasedonia waslavoni ni takriban theluthi mbili za wakazi wote. Robo moja ni Waalbania. Wengine ni mchanganyiko wa vikundi vidogovidogo kama Waturuki, Waromany, Waserbia na Wabosnia.
Wamasedonia wenyewe ni hasa Wakristo Waorthodoksi. Waalbania ni hasa Waislamu. Lakini zaidi ya theluthi ya watu wote husema ya kwamba hawana dini. Hii inaaminiwa ni urithi wa kipindi cha ukomunisti nchini.
Nchi na maeneo ya Ulaya | |
---|---|
Albania | Andorra | Austria | Belarus | Bosnia na Herzegovina | Bulgaria | Kroatia | Denmark | Estonia | Ufaransa | Hungaria | Iceland | Ireland | Italia | Latvia | Liechtenstein | Lithuania | Luxemburg | Masedonia | Malta | Moldova | Monako | Norway | Poland | Romania | San Marino | Serbia na Montenegro3 | Slovakia | Slovenia | Hispania | Ubelgiji | Uceki | Ufini | Ugiriki | Ujerumani | Uholanzi | Ureno | Urusi1 | Uswidi | Uswisi | Ukraine | Uingereza | Vatikan
Maeneo ya Ulaya ya kujitawala chini ya nchi nyingine: Visiwa vya Faroe | Gibraltar | Guernsey | Jan Mayen | Jersey | Isle of Man | Svalbard Nchi za Asia ambazo ni mwanachama wa baraza la Ulaya au vyombo vingine vya Ulaya: Armenia2 | Azerbaijan1 || Cyprus2 | Georgia1 | Kazakhstan1 | Uturuki1 Nchi zisizokubaliwa na umma wa kimataifa: Abkhazia | Nagorno-Karabakh2 | Ossetia ya Kusini | Transnistria | Jamhuri ya Kituruki ya Cyprus ya Kaskazini2 Maelezo: (1) nchi ya kimabara katika Asia na Ulaya; (2) nchi katika eneo la Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) lakini kiutamaduni huhesabiwa kuwa sehemu ya Ulaya; (3) Inaelekea kugawiwa kuwa nchi mbili za Serbia na Montenegro |