Sarafu
From Wikipedia
Sarafu ni kipande cha metali iliyotolewa na serikali ya nchi kama namna ya pesa. Mara nyingi sarafu ina umbo la duara kama kisahani. Kuna pia sarafu za pembe tatu, pembe nne au pembe zaidi.
Zamani sarafu ilikuwa umbo la kawaida ya pesa lakini siku hizi sehemu kubwa ya fedha inatolewa kama noti yaani kama karatasi. Karibu popote duniani sarafu hutumika kwa ajili ya pesa ndogo tu. Isipokuwa sarafu za dhahabu zinatolewa kwa idadi ndogo hasa kwa ajili ya watu wanaopenda kukusanya aina mbalimbali za sarafu zenye thamani ingawa hazitumiki kama pesa ya kulipia.
Makala hiyo kuhusu "Sarafu" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Sarafu kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |
Categories: Mbegu | Fedha