Nakuru
From Wikipedia
Nakuru ni mji wa Kenya ambao ni makao makuu ya mkoa wa Bonde la Ufa. Ikiwa na wakazi 289,000 (makadirio ya 2005) ni mji mkubwa wa nne nchini Kenya baada ya Nairobi, Mombasa na Kisumu. Iko kwenye kimo cha 1860 m juu ya UB katika mashariki ya bonde la ufa kando ya ziwa Nakuru.
Mji ulianzishwa mwaka 1904 na Waingereza kwenye njia ya reli ya Uganda. Kiasili eneo lilikuwa makao ya Wamasai waliopaita mahali "en-akuro" yaani mahali pa vumbi. Waingereza waliweka maeneo haya kando hasa kwa walowezi wazungu waliopewa mashamba makubwa. Nakuru ikawa kitovu cha "White Highlands" (Nyanda za juu za watu weupe).
Siku hizi Nakuru bado ni mji muhimu kwa kilimo cha mashamba makubwa yaliyo mkononi wa tabaka ya juu mpya ya Kiafrika tangu uhuru. Watalii wengi kidogo wanafika Nakuru wakitembelea hifadhi ya Nakuru ambayo ni karibu sana na mji mwenyewe.