Muskat (Omani)
From Wikipedia
Maskat (Kiarabu: مسقط) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Omani. Mji una takriban wakazi 650,000.
Maskat ina historia ndefu. Tangu karne ya pili ulijulikana kama bandari ya biashara ya kimataifa hasa ya uvumba.
1507 ilivamiwa na Wareno waliokaa hadi kufukuzwa mwaka 1649 na Sultani bin Saif. Baadaye mji ulishambuliwa na Waajemi pia na Waarabu Wahabiyya lakini Sultani Sayyid Said alifaulu kutetea utawala wake. Sayyid Said alihamisha baadaye mji mkuu wake kwenda Zanzibar. Tangu wakati ule mji ulirudi nyuma.
Serikali ya Sultani Qaboos bin Said iliweza kuboresha maisha ya wananchi tangu 1970 hasa kutokana na mapato ya mafuta ya petroli. Mji wa Maskat ulianza kukua na kupanuka sana