Luanda
From Wikipedia
Luanda (pia São Paulo de Luanda au Loanda) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Angola ikiwa na wakazi 2.776.125 (2005).
Contents |
[edit] Jiografia
Mji wa Luanda uko mkoani Luanda kaskazini ya mdomo wa mto Cuanza mwambaoni ya Atlantiki.
[edit] Wakazi
Kati ya wakazi milioni 2,7 walio wengi kabisa ni Waafrika wa makabila kama vile Waovimbundu, Wakimbundu na Wakongo. Lugha rasmi ni Kireno lakini lugha nyingi za kibantu zinatumika pia.
[edit] Historia
Mji ulianzishwa mwaka 1575 BK na Wareno kwa jina la São Paulo de Luanda. Imekuwa mji mkuu wa Angola tangu 1627. Hadi 1850 Luanda ilikuwa kitovu cha biashara ya watumwa kwenda Brazil.
Wakati wa uhuru mwaka 1975 wakazi wengi Wareno waliondoka mjini. Vita ya wenyewe kwa wenyewe katika Angola kati ya 1974 - 2002 ilileta hasara pia kwa ajili ya mji mkuu.
[edit] Uchumi
Luanda ni bandari muhimu nchini pia mwanzo wa reli kwenda Malange.