Kitigrinya
From Wikipedia
Kitigrinya (pia: Kitigray, Kitigre, Kihabesha) ni lugha ya Kisemiti inayozungumzwa katika Ethiopia (hasa jimbo la Tigray) na Eritrea.
Idadi ya wasemaji ni takriban milioni 5-6. Maandishi yake ni kwa alfabeti ya Kiethiopia. Kitigrinya imetoka katika lugha ya kale ya Ge'ez iliyokuwa lugha ya nyanda za juu za Ethiopia na hadi leo ni lugha ya liturgia katika kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia na Eritrea.
Katika Ethiopia Kitigrinya ni lugha ya tatu inayotumiwa na watu wengi (baada ya Kioromo na Kiamhari). Katika Eritrea ni lugha inatumiwa zaidi kabisa.