Werner Forssmann
From Wikipedia
Werner Forssmann (20 Agosti, 1904 – 1 Juni, 1979) alikuwa daktari mpasuaji kutoka nchi ya Ujerumani. Pamoja na kazi ya upasuaji alichunguza magonjwa ya moyo na ya mkojo. Alikuwa daktari mpasuaji mkuu katika hospitali za miji ya Dresden na Düsseldorf. Mwaka wa 1956, pamoja na Andre Cournand na Dickinson Richards alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.