Kireno
From Wikipedia
Kireno (Português - tamka "purtugesh") ni lugha ya lugha ya Kirumi iliyotokea nchini Ureno (Ulaya). Imekuwa lugha ya kimataifa kutokana na historia ya ukoloni ya Ureno yenye wasemaji wa lugha ya kwanza milioni 190, pamoja na wasemaji wa lugha ya pili kuna watu milioni 200 duniani wanaoelewana kwa Kireno.
Kutokana na historia ya ukoloni Kireno limepatikana katika nchi zifuatazo:
[edit] Kireno kama lugha rasmi:
- Ureno
- Brazil
- Angola
- Msumbiji
- Kabo Verde
- Guinea Bisau
- Sao Tome na Principe
- Timor ya Mashariki
[edit] Kieneo
- Makau (mkoa wa Uchina)
- Goa (mkoa wa India)
[edit] Historia ya lugha
Kireno ni moja kati ya lugha za Kirumi maana yake kimetokana na Kilatini cha Dola la Roma lililotawala eneo la Ureno kwa karne nyingi.
Ni karibu hasa na Kigalicia kinachozungumzwa katika Hispania ya Kaskazini.
Wareno waliacha lugha yao katika koloni zao. Leo hii idadi ya wasemaji katika Ureno ni milioni 10 tu - idadi kubwa kabisa wako nje ya Ureno hasa Brazil.
Ureno ilisambaa zaidi katika karne ya 20 kwa sababu Wareno waliondoka Ureno kutafuta kazi katika nchi nyingi za Ulaya. Vilevile kuna Wabrazil na Waangola waliotoka kwao kuhamia penginepo wakienda na lugha yao.